BODI YA FILAMU YAAHIDI USHIRIKIANO UANZISHWAJI WA MRADI WA TYEEO BARAZANI ENTERTAINMENT.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF) Bibi. Joyce Fissoo
Na: Frank Shija, MAELEZO
SERIKALI imepongeza juhudi za wadau wa Tasnia ya
Filamu nchini kutokana na jitihada zao katika kuhakikisha tasnia hiyo inakuwa
na kuwaletea maendeleo endelevu ikiwemo Ajira za uhakika kwa vijana.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mtendaji wa
Bodi ya Filamu Tanzania (KBF) Bibi. Joyce Fissoo alipokutana na ujumbe kutoka
Taasisi isiyo ya Kiserikali ya TYEOO walipomtembelea ofisini kwake jana kwa
ajili ya kutambulisha rasmiMradi wa TYEEO Barazani entertainment jana Jini Dar
es Salaam.
Fissoo alisema kuwa mradi huo ni muhimu kwa
mustakabari wa kukuza tasni ya Filamu nchini kwani utarahisha kufikisha katika
kuwafikia wadau wengi zaidi wa tasni hiyo walioko katika mikoa ya pembezoni.
“Niseme tu kwa dhati kabisa nawapongeza sana kwa
ubunifu wenu mradi huu ni mzuri na utaongeza tija katika tsni yetu ya Filamu,
name nina waahidi kuwapa ushirikiano pindi mtakapo kuwa mnahitaji”. Alisema
Fissoo.
Aidha alitoa ushauri kwa Taasisi hiyo kutumia
vibanda vya maonyesho ya Filamu vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini ili
kutekeleza mradi huo kwa kuwa nia ya Serikali ni kuona dhana ya urathimishaji
wa kazi za wasinii inafanikiwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TYEEO, John
Kallaghe amesema kuwa pamoja na kuwa mradi huo ni binafsi lakini kutokana na
imani kubwa waliyonayo juu ya Bodi ya Filamu wameona siyo busara kuendelea
kutekeleza jambo kubwa kama hili bila ya kushirikisha mamlaka hiyo ambayo ndiyo
msimamizi mkuu wa Tasnia ya Filamu nchini.
Aliongeza kuwa wazo la kuanzishwa kwa mradi huu
ilikuwa ni kusaidia kuwawezesha vijana kujikomboa katika lindi la umaskini
kupitia huduma itokanayo na mradi huu ambayo ni utayarishaji na usambazaji wa
kazi za wasanii wa Filamu kwa njia ya kisasa zaidi.
Kallaghe alisema kuwa wao kama wadau tasni hiyo
wako tayari kupokea ushauri na maelekezo ya namna ambavyo wanaweza kuboresha na
kutekeleza mradi huo kwa ajili ya maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Mradi wa TYEEO Barazani ni miongoni mwa miradi
kadhaa ambayo imeanzishwa na taasisi ya TYEEO, ulioasisiwa tangu mwaka 2013 na
unakadiriwa kutoa fursa ya ajira za uhakika kwa vijana takribani 6000 katika kada zote za Filamu hadi kufikia mwaka
2017.
No comments