NAIBU WAZIRI JAFFO: ELIMU YA JUU YA NCHINI KUWA NA SURA MPYA.
NAIBU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Selemain Jaffo amesema kuwa fursa za elimu ni nyingi katika
vyuo vya nje ya nchi na gharama zake ni nafuu.
Jaffo
ameyasema hayo wakati wa maonesho ya biashara ya Kimataifa katika
Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere (Sabasaba) katika banda la Global
Education Link (GEL), amewataka Watanzania kutumia maonyesho ya Sabasaba
kuwa ni kipindi muafaka kupata mambo mengi kwa wakati mmoja likiwamo
suala la elimu katika vyuo vya nje.
Jaffo amesema kuwa, maonesho ya sabasaba ni kipindi pekee kwa taasisi mbalimbali na huduma zake zinatolewa bure.Aidha
amesema kuwa wazazi wanaotaka kuwasomesha watoto wao katika vyuo vya
nje ya nchi kwa gharama nafuu watumie fursa hiyo kupita katika banda la
Global Education Link (GEL) watapata taarifa mbalimbali.
‘’Serikali
ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli imejipanga hivyo kama
wasaidizi wake lazima tujipange kuhakikisha kwamba tuangalie jinsi ya
kubadilika kwa kasi na kubadilika huko kwa kasi lazima tuhakikishe
tuna teknolojia ya kutosha kabisa kwanza kiushindani, tuanzishe vitu
ambavyo vitakuwa na soko kubwa”amesema .
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Education
link (GEL), Abdulmalik S.Mollel amesema kuwa vijana wanaopitia kampuni
yao hata baada ya kupata udahili na kwenda masomoni nje ya nchi, wana
utaratibu wa kufuatiliwa maendeleo yao ili mzazi aweze kuona thamani ya
fedha anayetoa kwa kusomesha mtoto nje ya nchi.
Mollel
amesema kuwa vyuo vya nje wanavyokwenda wanafunzi kuna wawakilishi
wanaofanya kazi moja kwa moja na GEL ya kufatilia mienendo ya wanafunzi
wao kwa kipindi chote wanachosoma na taarifa zao zinatumwa na kisha
mzazi kupewa taarifa za maendeleo ya mtoto.
Amesema
kuwa watoto wanaokwenda kusoma vyuo vya nje vinatambuliwa na TCU na
vinatambuliwa na bodi za nchi husika ili kuweza kumsaidia mtoto kuwa na
uhakika wa elimu na utaalam aliyopata katika vyuo hivyo.
Global
Education Link (GEL) inaangalia hali ya uchumi wa ndani kuwa mzazi
anaweza kumudu gharama hizo na hakuna tofauti na vyuo vya ndani.Anasema mtoto anayesoma nje wanaangaliwa kwa kila namna kuanzia ili kumuondolea mzazi usumbufu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Education
link (GEL), Abdulmalik S.Mollel akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Selemain Jaffo alipokuwa akiagana nae mara baada ya kulitembelea banda hilo
Baadhi ya Wadau mbalimbali wakiingia na kutoka ndani ya Banda hilio.
KUTOKANA
na uhitaji wa utaalam katika nchi katika kuelekea uchumi wa kati vijana
wanatakiwa kupata ujuzi na masomo hata katika vyuo vya nje.
Aliongeza
kuwa kuna fursa nyingi sio kwa serikali peke yake lakini hata kwa
wazazi wenyewe kutumia fedha zao kwa mambo ya msingi kuliko kufanya
harusi ya Sh. milioni 50 au milioni 100.Amesema
sh.milioni 50 zinazotumika katika harusi zinaweza kuziwekeza kwa vijana
wetu katika kuwapatia elimu iliyo bora zaidi kwa ajili ya uchumi wa
nchi yetu tunaweza kufanya vizuri zaidi.
Jaffo
amesema kuwa udahili wa wanafunzi katika vyuo vya ndani katika uhandisi,
Udaktari wa Binadamu ni chache kutokana na mfumuko wa ufaulu kwa kidato
cha sita pamoja na stashahada hivyo wanaweza kusoma katika vyuo vya nje
ambavyo vimeweza kuwekeza katika maeneo hayo.
“Leo
hii nikwambie ndugu tembelea katika kila siku za mapumziko fanya
tathmini kila harusi iliyopo inayofanywa na sisi wenyewe ndio
tunatengeneza harusi, unajikuta kumbe tungekuwa na mpango mkakati mzuri
wa kuhakikisha jinsi gani vijana wetu tunakuwa na wataalamu katika sekta
ya gesi, madini, kilimo pamoja na viwanda vidogo vidogo kwani kwa miaka
mitano wenzetu kutoka nchi mbali mbali watakuja kutuchukua".amesema
Jaffo.
Mollel
amesema kuwa watanzania kuondokana na fikra mgando kuwa wanaokwenda nje
ni watoto wa mafisadi hakuna kitu hicho na tunatakiwa kuondokana dhana
hiyo haitatusaidia kutokana serikali ilivyojipanga ya kuwa na wataalam
katika nyanja mbalimbali.
Gharama ya kusoma nchini China ni milioni nane kwa kozi ya udaktari ambapo unaweza kusoma nchini katika vyuo vya binafsi.Watoto
wanaokwenda kusoma vyuo vya nje vinatambuliwa na TCU na vinatambuliwa
na bodi za nchi husika ili kuweza kumsaidia mtoto kuwa na uhakika wa
elimu na utaalam aliyopata katika vyuo hivyo.
Global
inaangalia hali ya uchumi wa ndani kuwa mzazi anaweza kumudu gharama
hizo na hakuna tofauti na vyuo vya ndani kwa baadhi ya nchi.Anasema mtoto anayesoma nje wanaangaliwa kwa kila namna kuanzia ili kumuondolea mzazi usumbufu.
Mollel
amesema kuwa watanzania kuondokana na fikra mgando kuwa wanaokwenda nje
ni watoto wa mafisadi hakuna kitu hicho na tunatakiwa kuondokana dhana
hiyo haitatusaidia kutokana serikali ilivyojipanga ya kuwa na wataalam
katika Nyanja mbalimbali
Gharama ya kusoma nchini China ni milioni nane kwa kozi ya udaktari ambapo unaweza kusoma nchini katika vyuo vya binafsi.Makamu
wa Mkuu wa Chuo cha Mzumbe, Profesa Lugano Kusiluka alisema kuwa GEL
wanafanya kazi vizuri katika kufanya utaratibu wa vijana kutafuta vyuo
vya kusoma ambavyo vinatambulika na TCU.
Amesema
kuwa wanaona jinsi gani ya kushirikiana na GEL na Chuo cha Mzumbe
katika eneo la vyuo vya nje ili kuweza kufika sehemu nzuri kwa
kubadilishana uzoefu.Amesema
naye alishakwenda kusoma nje hivyo ameshauri vijana kutambua nini
wanaenda kufanya huku taifa likiwa linahitaji ujuzi wanaokwenda
kuchukua.
Baadhi
ya Wanafunzi waliosoma vyuo vya nje kwa kupitia GEL wamesema kuwa
utaratibu ni mzuri katika kuandaa mazingira na mawasiliano na vyuo
husika ambavyo wanakweda.Anita
Ituwe ,amesema kuwa wakati alipokuwa anatafuta jinsi ya kupata vyuo vya
nje walipata usumbufu lakini baada ya kufika GEL walipata maelezo ya
kutosha na kuweza kujiunga katika chuo kimoja nchini India.
Amesema
GEL wanaangalia hali ya uchumi wa ndani kuwa wazazi jinsi ya kumudu
gharama za masomo katika vyo hivyo ambavyo vinaratibiwa na GEL.Amesema
kuwa kuna mazingira bora ya kusoma vyuo vya nje kutokana uwekezaji kuwa
kila kitu kinachohitajika kwa mwanafunzi kinapatikana ndani ya chuo
bila kutoa gharama yeyote.
Nae
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Tanzania Taliki Abubakar ,amesema kwa
wakati alipokuwa anatafuta chuo cha kusoma alikuwa hana uhakika lakini
baada ya kukutana na GEL aliweza kupata Chuo cha kusoma na taratibu
zilikwenda haraka.
No comments