TAMKO LA MTANDAO WA MASHIRIKA YA WANAWAKE TZ, JUU YA USAWA KATIKA TEUZI ZINAZOENDELEA NAFASI ZA UONGOZI
Mkurugenzi
wa Mtandao wa jinsia nchini (TGNP) Liliani Liundi akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo Jijini Dar es salaam wakati
wakitoa tamko kuhusiana na teuzi zinazoendelea hususani katika nafasi
mbalimbali za maamuzi Serikali,
……………..
Mtandao wa Kijinsia Tanzania
(TGNP), kwa kushirikiana na wanaharakati wa maswala ya jinsia nchini wametoa
tamko kuhusiana na teuzi zinazoendelea hususani katika nafasi mbalimbali za
maamuzi Serikalini.
Akisoma tamko hilo kwa niaba
ya Mashirika hayo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji TGNP, Lilian Liundi
amesema licha ya wanawake kuwa zaidi ya asilimia 50 ya Watanzania wote
chakusikitisha uwakilishi wao katika
nafasi za maamuzi umekuwa ukishuka kila kukicha.
Amesema wamekuwa mstari wa
mbele tukipaza sauti kuhusu teuzi ambazo kwa sehemu kubwa zimekuwa hazizingatii
usawa wa kijinsia na kutolea Mfano, katika Baraza la Mawaziri kati ya mawaziri
19 wanne tu ndio wanawake ambayo ni asilimia 21.1 ukilinganisha na uteuzi wa
mwaka 2015 ambapo wanawake walikuwa 10 sawa na asilimia 33.3.
Bi, Liundi ameongeza kuwa
ikumbukwe kwamba Tanzania ni moja kati ya Mataifa yaliyosaini mikataba
mbalimbali ya Kimataifa inayoweka misingi ya usawa jinsia kwa binadamu hususani
haki ya kushiriki nafasi yoyote ya uongozi.
Amesema wanatoa ushauri kila
uteuzi unapofanyika wanaopanga majina ya walioteuliwa wabainishe kama ni
mwanaume au mwanamke ili kurahisisha utambuzi wa wachambuzi.
Aidha bi liundi ameongeza
kuwa Mtandao wa Mashirika ya utetezi wa haki za wanawake nchini wataendelea
kusimama imara kupaza sauti zao hususani katika teuzi zinazoendelea kufanyika
ikiwa ni pamoja na kushirikiana na serikali ya awamu ya tano katika kuleta
maendeleo ya Taifa.
No comments