Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) umeandaa mafunzo ya siku tano kwa
madiwani kutoka kata zaidi ya 20 nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu
maswala mazima ya bajeti pamoja na kufatilia jinsi bajeti inavyotoka na
kutumika hususani kwenye mlengo wa kijinsia.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa jinsia
Tanzania (TGNP) Bi,Liliani Liundi amesema lengo la kuanda mafunzo hayo ni kuwajengea
uelewa mpana viongozi hao kuhusu maswala mzima ya bajeti hili kuwawezesha kutimiza
wajibu wao kwa ufanisi.
Amesema mafunzo
hayo pia yamelenga kuwawezesha viongozi hao kutambua haki za makundi mbalimbali
katika jamii pamoja na namna ya kuitumia Bajeti hiyo katika kuwasaidia wananchi
hasa makundi makundi maalum yaliyopo katika jamii zao.
Aidha Bi liundi ameongeza kuwa mafunzo hayo pia yatawawezesha madiwani
hao kuwa na uelewa mpana zaidi kuhusu dhana ya bajeti ya mlengo
wa kijinsia ambayo amesema ni
bajeti inayopanga Rasilimali kulingana na makundi mbalimbali yaliyopo katika
jamii zetu hivyo kuwa ni bajeti ya haki kwa wananchi wote.
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamesema mafunzo
hayo yamekuja wakati muafaka ambapo bajeti ya Tanzania imesomwa tayali wao
wakiwa kama viongozi wa ngazi za chini ambao ndio walengwa wa bajeti hiyo
mafunzo hayo yatawasaidia katika utendaji wao hasa katika utekelezaji wa
majukumu yao kwa wananchi.
No comments