KIWANDA CHA CHUMA CHA MMI STEEL DAR CHATOZWA FAINI MIL 10
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akisaini kitabu cha wageni
muda mfupi baada ya kuwasili katika Ofisi ya Serikali ya mtaa wa (TPDC)
alipofanya ziara
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.
Luhaga Mpina akisikiliza maelezo kutoka kwa mwenyekiti wa serikali za
mtaa wa (TPDC)Bw, Idrisa Hashimu kuhusu Uchafuzi wa Mazingira
Unaofanywa na viwanda katika mtaa huo.
Naibu
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga
Mpina akiwa katika ukaguzi wa Mazingira katika kiwanda cha MMI steel
kinachotuhumiwa Kuchafua mazingira katika mtaa wa TPDC.
……………………………………………………………………………………………………………..
EVELYN
MKOKOI -DAR ES SALAAM
Kiwanda
cha kutengeneza vyuma cha MMI Steel kilichopo katika eneo la viwanda mikocheni
jijini Dar es Salaam, kimetozwa faini ya shilingi milioni kumi na kutakiwa
kulipa faini hiyo baada ya siku saba kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira na
kanuni zake ya mwaka 2004, kwa kutiririsha maji machafu katika maeneo ya mtaa
wa TPDC kwa warioba jijini dar es salaa. Maji ambayo ni hatari kwa mazingira na
viumbe hai.
Adhabu
hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Mhe. Luhaga Mpina alipotembelea eneo la mtaa wa viwanda mikocheni
kufuatia uchafuzi wa mazingira unaotokanao na utitiririshaji wa majitaka katika
maeneo hayo.
Wakati
huohuo, Shirika la maji safi na majita taka Jijini Dar es Salaam na Pwani
( Dawasco) limepewa siku kumi na saba kumaliza tatizo la utiririshaji wa
maji taka katika mtaa wa TPDC mikocheni kwa Warioba jijini Dar es Salaam.
Maagizo
hayo yametolewa na Naibu Waziri Mpina Baada ya kufanya usafi jumamosi ya mwisho
wa mwezi wa tatu na kutoa siku saba kwa DAWASCO na NEMC kusimamia suala zima la
usafi wa mazingira na agizo lake kuupuzwa.
Awali,
Mhe. Mpina alisema kuwa uchafuzi wa mazingira hauwezi kuendelea kuvumiliwa na
lazima hatua za kisheria zichukuliwe, na kuwaasa watendaji wa taasisi za
serikali kuyapa kipaumbele maagizo yanayotolewa na viongozi wa ngazi za juu za
serikali kinyume na hapo ni kutokutii mamlaka. “tasisi za serikali lazima
zifanye kazi kwa kushirikiana kutokana na kwamba kumekuwa na kutupiana mpira
kati ya NEMC, dawasco na Manispaa ya kinondoni katika suala zima la utatuzi wa
uchafuzi wa mazingira katika mtaa wa TPDC.” Alisema.
Naibu
waziri Mpina aliongeza kuwa ifikapo tarehe 30/7/2016 asikutane tena
na tatizo la uchafu na harufu mbaya katika mtaa wa TPDC kwani hali hiyo ni
hatari sana kwa afya ya wakazi wa maeneo hayo na mazingira.
Kwa
upande wake DAWASCO ikiwakilishwa na Injinia Erick Jackson alisema kuwa Tangu
muheshimiwa Naibu Waziri Mpina atoe agizo la uondoshwaji wa majitaka na
uboreshwaji wa miundombinu katika mtaa huo, wamekuwa wakifanya kazi na bado
inaendelea na kazi hiyo pamoja na kukabiliwa na changamoto mbalimbali za
kifedha na ufundi.
Hata
hivyo uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya kinondoni umelishitaki shirika la
maji safi na maji taka jijini dar es salaam na Pwani DAWASCO ,kiwanda cha MMI
steel na Tembo Tiles kwa uchafusi wa mazingira kwa kutirirsha maji taka.
No comments