AZANIA BANK YATOA MADAWATI 75 KONDOA
Mkurugenzi
Uendeshaji wa Azania Bank, Nurdin Semnangwa akizungumza katika hafl
fupi ya kukabidhi hundi ya shs. milioni 6 kwa Mfuko wa Maendeleo wa
Kondoa (KDF) jijini Dar es Salaam itakayosaidia ununuaji wa madawati
katika Wilaya za Kondoa na Chemba mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa
Kondoa (KDF), Balozi mstaafu Cyprian Majengo kwa ajili ya kununulia
madawati katika Wilaya za Kondoa na Chemba. Hafla ilifanyika jijini Dar
es Salaam .
Mkurugenzi
Uendeshaji wa Azania Bank, Nurdin Semnangwa (katikati) akizungumza
katika hafla ya kukabidhi hundi ya Shs milioni 6 kwa Mfuko wa Maendeleo wa Kondoa (KDF).
Mkurugenzi Uendeshaji wa Azania Bank, Nurdin Semnangwa (wa pili kulia), akimkabidhi mfano wa hundi ya Shs. Milioni 6 Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa Kondoa (KDF), Balozi mstaafu Cyprian Majengo.
Kukabidhi mfano wa hundi.
Mkurugenzi Uendeshaji wa Azania Bank, Nurdin Semnangwa (katikati), akimkabidhi hundi ya Shs. Milioni 6 Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa
Kondoa (KDF), Balozi mstaafu Cyprian Majengo kwa ajili ya kununulia
madawati katika Wilaya za Kondoa na Chemba. Hafla ilifanyika jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Mweka Hazina wa KDF, Abdilay Mvula.
Mkurugenzi Uendeshaji wa Azania Bank, Nurdin Semnangwa (kulia),akimkabidhi mfano wa hundi ya Shs. Milioni 6 Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa
Kondoa (KDF), Balozi mstaafu Cyprian Majengo kwa ajili ya kununulia
madawati katika Wilaya za Kondoa na Chemba. Haflailifanyika jijini Dar
es Salaam.
NA MWANDISHI WETU
BENKI
ya Azania Ltd imetoa madawati 75 kwa Mfuko wa Maendeleo wa Kondoa (KDF)
ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kila mwezi kutoa sehemu ya mapato
kwa ajili ya kusaidia jamii.
Akizungumza
katika hafla ya utoaji wa madawati hayo iliyofanyika jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Benki ya Azania, Nurdin Semnangwa,
alisema: “Mwaka huu kwa kuitikia mwito wa kilio cha madawati kwa
wanafunzi wetu wa shule za msingi na sekondari, benki ya Azania
ilidhamiria kuhakikisha wanafunzi 1,200 wanapata madawati ya kukaa.”
Aidha,
Semnangwa aliongeza: “Leo tunatoa kiasi cha shilingi milioni sita
kuweza kuondoa tatizo la kukaa chini wakati wa masomo ili yapatikane
madawati 75…kwa watoto 225 wa wilaya za Kondoa na Chemba.” Semnangwa
alisisitiza kwamba utoaji wa madawati utaendelea katika siku za usoni
kwenye mikoa ya Geita, Mwanza, Simiyu, Songwe na Dar
es Salaam kwani walishafanya Kilimanjaro.
es Salaam kwani walishafanya Kilimanjaro.
“Madhumuni yetu ni kuendelea kujitolea sehemu ya faida kwa jamii ya Watanzania wakati wowote,”
alisisitiza Mnangwa.
alisisitiza Mnangwa.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa KDF, Balozi mstaafu Cyprian Majengo alisema:
“Tunaishukuru Benki ya Azania, asasi hii imekuwa ikishughulika na wilaya
zote mbili (Kondoa na Chemba) kwa kuzingatia hilo msaada huu utapelekwa
kwenye maeneo hayo.”
“Tangu
kusajiliwa kwake (2002) asasi imesaidia mambo mengi katika kuleta
maendeleo ya wilaya zote mbili…ujenzi wa madarasa kwa kutoa vifaa vya
ujenzi, kutafuta bei nzuri ya zao la mbaazi, alizeti na ufuta, kupeleka
walimu wa muda kutoka vyuo vikuu wakati wa likizo katika shule za
sekondari,” alisema Majengo.
Hata
hivyo alitoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kwa wingi
kuitazama jamii hususan kwa changamoto ya sasa ya ukosefu wa madawati
katika shule za msingi na
sekondari.
sekondari.
(Picha na Francis Dande)
No comments