TAMASHA LA MTOKO WA PASAKA KUFANYIKA APRILI 20 MWAKA HUU
Dar es salaam - Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao imesema itashiriki kikamilifu katika maandalizi ya Mtoko wa Pasaka utakaofanyika Aprili 20,2025, katika Ukumbi wa The Superdome Masaki Jijini Dar es Salaam ambapo lengo kuu ni kuwakutanisha watanzania kifurahia kupitia nyimbo,maombi na kutoa msaada kwa wakina mama wajawazito.
Hayo yamebainishwa na leo Aprili 7,2025 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Steven Nyerere wakati akizungumza na wanahabari amesema tukio hilo litakuwa la kiroho na kihistoria kwani litaliombea Taifa pamoja na kumuombea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika mwaka huu wa uchaguzi Mkuu.
Aidha,ameeleza kwamba mambo yatakayolipamba tukio Hilo ni maonesho ya muziki wa Injili,yatakayoongozwa na mwanamuziki mashuhuri Christina Shusho,ambaye ni mwanachama wa Mama Ongea na mwanao,Shusho atapanda jukwaani pamoja na wanamuziki wengine kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania.
"Mtoko huu utakuwa wa kipekee sana,ni mwaka wa tati kushiriki,Nia na madhumuni ni kuwaunganisha watanzania na Afrika Mashariki katika amani na mshikamano,pia kuwaombea viongozi wa Taifa". Alisema Shusho.
Hata hivyo amesisitiza kwamba maombi na mshikamano ni njia ya kulinda amani ya nchi,Kauli mbiu ya Mwaka huu:"Kwa Maombi Utashinda",
Post Comment