Breaking News

WATUHIMIWA 25 WADAKWA KWA MAKOSA YA KIMTANDAO

Na Neema Mpaka - Jeshi la polisi kwa kushirikiana na mamlaka zingine za kisheria ikiwemo mamlaka ya mawasiliano (TCRA) wamefanikiwa kuwakamata wahutumiwa 25 wanaojihusisha na makosa ya kimtandao katika maeneo mbalimbali ya jijini dare es salaam na mikoa mwingine.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo jijini dare es salaam kamanda wa polisi Kanda maalum ya dare es salaam Jumanne Muliro amesema wahutumiwa hutumia laini za simu zisizo na usajili wao, kuingilia na kubadili namba za utambuzi halisi wa simu.

Aidha amesema wahutumiwa hujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu na kujifanya maafisa wa mfuko wa pesheni na kuwaibia wastaafu.

"Wahutumiwa hujipatia pesa kwa kutuma ujumbe kama 'tuma Ile hela kwenye namba hii,tuma kwenye namba hii Ile pesa ya kodi', lete namba ya NIDA, vitambulisho tukushughulikie mapunjo Yako ya kustaafu"amesema Muliro.

Aidha amewataja waliokamatwa ni pamoja na Kelvin Sauro mkazi wa ifakara na wenzake 14, Baruani Hamisi Katema maarufu Majani mkazi wa kahororo mkoa wa Kagera na wenzake wa nne.

"Baadhi ya wahutumiwa wamekamatwa kwa kuwa na vifaa vya kielekroniki kuhusiana na makosa Yao kama simu janja10, simu za kawaida 26 , laini za simu 84 za makampuni mbalimbali,
 memory kadi 2, kompyuta mpakato 1, mashine ya kusajili laini 2 na funguo moja ambayo ni mazalia ya uharifu wao" Amesema Muliro.  

Amesema baadhi ya wahutumiwa tayari wamefikishwa mahakama ya kisutu na wengine taratibu za kisheria zinakamilishwa ili wafikishwe mahakamani.

Kadhalika jeshi la polisi linatoa wito kwa wananchi kufuata Sheria na kanuni za matumizi ya mitandao na pia kuwataadharisha wananchi kutokutoa vitambulisho vyao kama vya NIDA na vingine kwa watu wasiowajua. Lakini pia jeshi la polisi linatoa onyo Kali didhi ya wote wanaojihusisha na makosa ya mitandao na mengine kwani watashughulikiwa vikali lakini kwa mujibu wa Sheria.

Wakati huo huo kamanda Muliro amesema jeshi limejiandaa vizuri kuweka mazingira ya kiusalama katika mchezo wa soka kati ya timu ya simba na yanga utakaochezwa kesho majira ya saa moja usiku.

"Hatuta ruhusu mtu yeyote kwenda kwenye mchezo huo akiwa na silaha ya aina yeyote isipokuwa watu wachache wenye mamlaka ya kisheria ambao wanashughulika na masuala ya kiusalama, lakini pia chupa, na vilevi havitaruhusiwa uwanjani"Amesema kamanda Muliro.

Aidha amesema watu wasiende kwenye mchezo huo wakiwa na matokeo Yao mfukoni na matokeo yeyote yatakayotokea yakubaliwe na isiwe kigezo Cha chanzo Cha Fujo katika mchezo huo.

No comments