WANANCHI JITOKEZENI UCHUNGUZI WA AFYA YA KINYWA NA MENO TEMEKE HOSPITAL

Dar es salaam - Wananchi wa Wilaya ya Temeke na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke kushiriki maadhimisho ya Siku yaAfya ya Kinywa na Meno ambayo huadhimishwa kila tarehe 20 Machi kila mwaka.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Afisa Uhusiano wa Hospital ya Rufaa ya Temeke Bwana Onesmo Milanzi alisema madaktari Bingwa wa Kinywa na Meno wanawakaribisha wananchi wote kushiriki katika zoezi hilo.

"Madaktari wetu bingwa wa kinywa na meno wanawakaribisha wananchi wote kufika katika idara ya Kinywa na Meno na kupata huduma za uchunguzi wa Kinywa na Meno pamoja na elimu ya Afya ya Kinywa na Meno bure na watakaobainika kuwa na changamoto watapatiwa matibabu kwa utaratibu wa kila siku wa Hospitali," alisema Milanzi.

No comments