WAKALA WA MISITU WAPANDA MITI 1,6000 KIBAHA KUADHIMISHA SIKU YA MISITU DUNIANI

Kibaha, Machi 21, 2025 – Katika kuadhimisha Siku ya Upandaji Miti Kitaifa na Siku ya Misitu Duniani, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Mashariki wamepanda miti ya mikaratusi 1,600 katika eneo la Kidimu, Wilaya ya Kibaha, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhifadhi mazingira.

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nikson John, aliwapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo, akisisitiza umuhimu wa kushirikiana na TFS katika kutunza mazingira.
Kwa upande wake, Kamanda wa Kanda ya Mashariki, PCO Mathew Ntilicha, akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi, Prof. Dos Santos Silayo, alisema lengo kubwa la zoezi hilo ni kuhamasisha jamii kuhifadhi misitu kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.

Maadhimisho haya, yanayofanyika Machi 21 kila mwaka, kwa 2025 yamebebwa na kaulimbiu: “Ongeza Thamani ya Mazao ya Misitu kwa Uendelevu wa Rasilimali za Misitu kwa Kizazi cha Sasa na Kijacho.”





No comments