RC CHALAMILA AZINDUA RASMI BIASHARA SAA 24 JIJINI DAR
Mkuu wa mkoa wa dare salaam mheshiwa Albert Chalamila amemtaka katibu tawala wa mkoa kuandaa safari maalumu ambayo itahusisha jumuiya ya wafanyabiashara karikoo pamoja na wakuu wa wilaya waende kufanya matangazo katika nchi za Lusaka, Zambia, Lilongwe Malawi, Congo, Rwanda na Burundi ya kutangaza kuwa karikoo imekucha sasa ni masaa 24
Akizungumza wakati wa sherehe za uzunduzi wa ufanyaji biashara wa saa 24 uliofanyika katika soko la karikoo
Amesema jumuiya ya wafanyabiashara 10 pesa zao za nauli zinatoka ofisi ya mkuu wa mkoa waende wakainadi nchi ya Dokta Samia Suluhu Hassan.
Aidha mkuu wa mkoa amesema wiki ijayo atakaa na wanajumuiya ya wafanyabiashara wa karikoo ili kuona namna ya kuweka mpango wa kuanza kuwakopesha bidhaa vijana wote wanaotaka kuanza kufanya biashara na wao viongozi ndio watakuwa wadhamini wao.
"Vijana wote waliomaliza vyuo waache kulia wakiwa nyumbani waje dares salaam tukae na wafanyabiashara wa nguo, viatu, vifaa vya ujenzi waandae mpango wa kuwakopesha bidhaa na kurejesha kadri wanavyouza. amesema mkuu wa mkoa"
Kadhali amesema ameawaomba wafanyabiashara kuweka mpango wa kuwa na punguzo maalumu hasa kwa wale watakao Kuja kununua bidhaa kuanzia saa sita ya usiku mpaka saa kumi na moja alfajiri.
"Nitayaomba makampuni ya simu kuweka punguzo ama kuweka Wi-Fi Bure katika maeneo yote ya karikoo kuanzia saa sita usiku mpaka saa kumi na moja asubuhi, lakini pia nitaongea na baadhi ya mabenki ili kuona namna ya kupunguza riba kwa wale wafanyabiashara waliokubali kufungua biashara kwa saa 24, Gavana wa Benki kuu ya Tanzanzia (BOT) ameshawapatia kibali Cha kuruhusu mabenki yote kwa wale watakao kubali kufanya biashara masaa 24 wafanye biashara. Amesema Chalamila"
Aidha amesema ametoa maelekezo kwa wasaidizi wake hasa katibu tawala wa mkoa wiki ijayo ataunda kamati ya kupitia upya Sheria ndogo ndogo za almashauri zinazokinzana na wafanyabiashara wa saa 24 pamoja na kumshauri waziri wa tamisemi ili kuona namna tunavyoweza kuziondoa na kuruhusu watu wafanye biashara masaa 24.
Amesema maeneo mengine yatakayofungua biashara saa 24 ni pamoja na Mwenge, Manzese, Tandika, Mbagala, Ubungo na Magufuli bus stand.
Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa dare es salaam doktaToba Nguvila amesema pamoja na kuruhusiwa kufanyika kwa biashara kwa saa 24 Bado kamera hazijafungwa ambapo zoezi la ufungaji katika soko hilo linatarajiwa kuanza mapema march 1 mwaka huu.
"Wakala wa ufundi na umeme Tanzania (Temesa) tayari wameshasaini mkataba na almashauri ya jiji la dares salaam (ilala) kufunga kamera 40 za usalama katika soko la karikoo shughuli hii inatarajia kuanza mapema mwenzi march tarehe 1 2025 ikiwa na jumla ya bajeti ya Bilioni mia Tano na kumi na nne hii itasaidia kwa ajili ya kuangazia usalama wa watu na Mali zao hasa wakati wa kuangalia makosa mbali mbali kwa vyombo vya usalama itakuwa rahisi kuwabaini waarifu. Amesema Toba"
Aidha amesema katika kuboresha miundombinu ya umeme shirika la umeme la Tanzania limeanza kubadilisha nguzo za umeme kutoka za miti kwenda za zege katika eneo la karikoo, pamoja na kubadilisha nyaya za wazi na kuweka zilizofunikwa hadi sasa kazi ya kubadilisha nguzo imekamilika kwa asilimia 90 na za kubadilisha nyaya imekamilika kwa asilimia 95.
No comments