DKT. BITEKO ATOA RAI KWA WATANZANIA KUTUNZA NA KULINDA VYANZO VYA MAJI

Dar es salaam - Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Dotto Biteko, ametoa rai kwa Watanzania kutunza na kulinda vyanzo vya Maji kwa kuwa ni Jukumu la kila mtu ili viweze vyanzo hivyo viweze kutoa Maji kwa muda mrefu na Uhakika.

Dkt. Biteko ameyasema hayo leo, Machi 19, 2025 kwenye Uzinduzi wa Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Maji kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 Katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar Es salaam.

Dkt. Biteko amesema Vyanzo vya Maji visipotunzwa tutapata Changamoto ya Maji baadae huku akiitaka Jamii kutunza usafi wa Mazingira na kulinda vyanzo vya Maji na kutunza maeneo yote ya kuhifadhi Misitu.
Aidha Dkt. Biteko amesema Ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi Imetoa maelekezo katika kipindi cha Miaka mitano ijayo lengo lla Chama hicho ni kuona kuwa nchi inaendelea kuwa na Usalama wa Maji na huduma ya Maji na kuwafikia Wananchi wa Vijijini zaidi ya Asilimia 85 na zaidi ya Asilimia 95 ya Wakazi wa Mijini ifikapo Mwaka 2025.

Akielezea Hali ya upatikanaji wa hali ya Maji kwasasa Nchini Dkt. Biteko amesema hadi sasa hali ya upatikanaji wa Maji Mjini ni Asilimia 84 na Vijijini ni Asilimia 79 taarifa hii inaonyesha kuwa tumepiga hatua kubwa katika kuwaunganisha watu kwenye Maji ukilinganishwa na mwaka 2022/23,".
Hata hivyo Dkt. Biteko amezipongeza sana Mamlaka za Maji pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa hatua hiyo waliyofikia.

"Lakini yapo maeneo ambayo tulipiga hatua kubwa moja wapo ni ongezeko la uzalishaji Mkubwa wa Maji kwa Takribani asilimia 7 kutoka ujazo wa Mita za Ujazo Milioni 593 hadi kufikia milioni 685 kwa Mwaka huu 2023/24,".



No comments