ALAT YAOMBA WIKI YA SERIKALI ZA MITAA, KUTANGAZA FURSA NA MAFANIKIO YAKE
Na Neema Mpaka, Dar es salaam - Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ,Murshid Ngeze amemuomba Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania,Dkt
Samia Suluhu Hassan kuwa na wiki ya serikali za mitaa ili waweze kuonyesha shughuli mbalimbali zinazofanywa pamoja na kutangaza mafanikio ya mamlaka hizo.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa ALAT, Nzege leo Machi 19,2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, amesema kwamba wiki ya serikali za Mitaa ni Moja ya fursa kwa wananchi waweze kutambua na kujionea fursa zinazopatikana kwenye Halmashauri za mitaa.
Aidha , amesema katika wiki ya serikali za Mitaa tutaalika mashirika mbalimbali kutoka nje ya nchi, wafanyabiashara, makampuni mengi yanayofanya kazi na haya yataleta fursa kwa wananchi waweze kupata ujuzi na wiki hii itafanyika kila mwaka na italeta fursa mbalimbali za kiuchumi na kufungua milango ya kiuchumi.
"Wiki ya Serikali za mitaa fursa mojawapo ya kufungua uchumi kwenye maeneo yetu", Amesema Ngeze.
Hata hivyo,amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassa kukubali kufika kwenye mkutano wa 39 wa ALAT uliofanyika Mkoani Dodoma ambapo mkutano huo ulikuwa na kauli mbiu "Shiriki Uchaguzi 2025 kwa Maendeleo Endelevu",
"Tunamshukuru Rais kufika kwenye mkutano wa ALAT na akaweza kutuambia yale aliyokua ameahidi mwaka 2021 wakati anatufungulia mkutano wa Uchaguzi kuwa ametekeleza kwa kujenga madarasa zaidi 13,000, ujenzi wa vituo vya afya kwenye wilaya mbalimbali,ujenzi wa Vyuo vya VETA kila mkoa yote ametekeleza", amesema
Pia Mwenyekiti Ngeze amewashukuru wadau mbalimbali kwa ushirikiano wao walioutekeleza kwa kufanikisha mkutano huo.
Vile vile amesisitiza kuwa maagizo yaliyotolewa na Rais ni kama ifuatavyo,kuendelea kwa kusamia kwa umakini ukusanyaji wa mapato pamoja na kubana matumizi kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi.
Ameendelea kwa kusema kwamba Halmashauri ziendelee kuweka mipango inayoendana na mpango wa 2025/2050.
Alieleza kwamba kuendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa ajili ya kuwa na mapato mengi,pia kusimamia Sheria kwenye Mamlaka zetu hasa vibali kwenye ujenzi na Sheria kwa wawekezaji.
Amebainisha kwamba kutenga maeneo mahususi kwa ajili ya uwekezaji yabaki kwa ajili hiyo pamoja na kwenda kuwaeleza wananchi miradi yote iliyotekelezwa na Halmashauri .
Sambamba na hayo yote ametoa wito kwa madiwani kufanya mikutano ya hadhara ili kuwaeleza wananchi yaliyotekelezwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Alimalizia kwa kusema kwamba ALAT imejiwekea mikakati ya kujengaa jengo la kitega uchumi lenye ghorofa 4 Ofisi pamoja kumbi za mikutano.
Post Comment
No comments