RC CHALAMILA AKUTANA NA KAMISHNA WA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA)
Dar es salaam - Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Februari 18, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bwana Yusufu Mwenda katika ofisi ya mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt. Toba Nguvila na viongozi wengine amefanya mazungumzo na Kamishna huyo pamoja wataalamu wenginge waandamizi wa Mamlaka hiyo ya Mapato.
Katika mazungumzo yao pamoja na mambo mengine RC Chalamila amezunguzia mkakati wa Mkoa kufanya biashara saa 24 katika maeneo mbalimbali ya Mkoa yaliyoainishwa, ambapo kwa upande wa TRA ni fursa adhimu itakayopelekea Mamlaka hiyo kukusanya mapato zaidi ukilinganisha na sasa.
No comments