KAWAIDA: AJENDA YA MITANO TENA NI DKT. SAMIA NA DKT. MWINYI TU, VIJANA TWENDE TUKAGOMBEE
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC) amewatoa hofu vijana ambao wanataka kuwania nafasi za udiwani, ubunge na uwakilishi kuwa wakae tayari kuwani nafasi hizo kwakuwa ajenda ya Mitano Tena ni kwa Mgombea wa Urais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea wa Urais Mteule wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Ndg. Kawaida amesema hayo wakati akizungumza mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Chuo cha UVCCM cha Tunguu alipoenda kuweka jiwe la msingi.
"kumezuka tabia kwa Wawakilishi, Wabunge, ajenda ya mitano tena ilikuwa ya wawili tu Mwenyekiti wetu wa CCM na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar. Wasiwatishe vijana kuwa wao mitano tena, vijana nendeni mkagombee," amesisitiza Ndg. Kawaida
No comments