JESHI LA POLISI WAFANYA UKAGUZI WA MAGARI YA SHULE ZA UDEREVA NA KUTOA ELIMU KUHUSU MFUMO MPYA WA LESENI
Na. Abel Paul, Jeshi la Polisi Arusha - Katika kuhakikisha Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani¹10 Mkoa wa Arusha unaendelea kudhibiti ajali zinazosababishwa na madereva wasio na sifa na wasio fuata sheria limeungana na Mamlaka ya Mapato Tanzania kutoa elimu kwa shule za udereva Mkoani humo huku likitoa ufafanuzi na elimu juu ya mfumo mpya wa leseni za Udereva.
Akiongea na wamiliki na walimu wa shule za udereva Mkoani Arusha Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amesema kuwa leo februari 18,20225 wamekutana wamiliki na walimu wa shule za udereva Mkoani humo lengo likiwa ni kutoa elimu, ukaguzi wa vyombo, kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mfumo wa upatikanaji wa leseni
SSP Zauda ameongeza kuwa kutokana na mabadiliko hayo ya mifumo ya tehama katika utoaji wa leseni kikosi hicho kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) waliona ni vyema kuwaita wamiliki wa shule za udereva ambao ndio wadau wakubwa wa uzalishaji wa madereva bora Mkoani humo ili kuwapa elimu hiyo na mabadiliko ya mfumo huo.
Sambamba na hilo akatoa wito kwa wamiliki wa shule za udereva kufika kwa wakati kikosi cha Usalama barabarani kupata elimu na mabadiliko hayo ya mfumo mpya wa leseni ili kuendelea kuzalisha madereva makini wenye kukidhi vigezo vya kitaifa na kimataifa.
Justine Mkutwa ambaye ni afisa kodi mwandamizi kutoka mamlaka ya mapato Mkoa wa Arusha akawaomba wamiliki na walimu wa shule za udereva kuupokea kwa mikono miwili mfumo huo mpya wautoaji leseni wenye lengo la kuleta ufanisi wa utoaji wa leseni kwa madereva waliopata ujuzi wa udereva katika Daraja husika huku akiweka wazi kuwa mfumo huo unamtaka mteja mwenyewe ajihudumie.
Nae Athumani Walele ambae ni mkufunzi wa shule ya udereva new world licha kupongeza Jeshi la Polisi na mamlaka ya mapato (TRA) kuja na mfumo mpya wa utoaji leseni amebainisha kuwa utakuwa chachu ya kuletea madereva wenye ufanisi na ujuzi ambao wanazingatia sheria za usalama Barabarani.
Kwa upande wake Anna Makundi ambaye ni Mkufunzi wa Shule ya udereva Modern amesema elimu na ukaguzi wa vyombo vyao umewapa ari mpya ya kiutendaji huku akishukuru kuja na mwaarobaini wa kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa madereva bora ambao wataleta sifa ndani na nje ya nchi.
Lameck Yona Kaimu Msajili kutoa chuo cha veta Arusha akasisitiza kuwa mfumo huo utachangia Uchumi wa taifa kukua ambapo amebanisha kuwa mfumo huo utatoa madereva sahihi watakaotumia vyombo kwa usahihi na kufuata sheria za usalama Barabarani na kupunguza ajali ambazo zimekuwa zipoteza nguvu kazi ya taifa.
No comments