DC MPONGOLO AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM ILALA
Dar es salaam - Mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpongolo leo Februari 21, 2025 amewasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha Desemba 2024 mpaka February 2025 kwa Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Ilala ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Alhaji Said Side.
Akizungumza wakati akiwasilisha ilani hiyo amesema Ilani hiyo unalenga kuelezea mafanikio ya miaka 4 ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kipindi hicho imeweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hususani katika sekta Afya, Elimu, Maji na Miundombinu.
Nianze kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kushusha shilingi bilioni 347 za Maendeleo kwa ajili ya miradi mbalimbali ndani ya wilaya llala.
"Wilaya ya Ilala Tunamshukuru Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametupatia shilingi bilioni 347 za miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya sekta ya Elimu na Miundombinu ya barabara" alisema Mpogolo.
Alisema wilaya ya Ilala wanajivunia mafanikio makubwa ikiwemo jitihada za Halmashauri ya jiji katika uongozi wa awamu ya sita ikiwemo ujenzi wa magorofa nane ya shule za Sekondari ambayo yapo katika hatua mbalimbali kwa gharama bil 14.4 na mradi mwingine wa magorofa kumi anaotarajiwa kujengwa kwa bilion 18 sambamba na kuajili walimu wapya 124 wa mkataba.
Akizungumzia sekta ya afya katika kipindi cha miaka minne sekta ya afya inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa mujibu wa maelekezo ya Ilani ya chama cha Mapinduzi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ibara ya 83, utekelezaji huo ni sehemu ya kuboresha miundombinu ya afya ikiwa ni pamoja na kukarabati miundombinu chakavu, ujenzi vituo vipya vya afya na ununuzi wa vifaa tiba.
Aidha DC Mpongolo ametaja mafamikio mengine wanayojivunia Ilala ni upande wa miundombinu barabara za kisasa zinazojengwa kwa kushirikiana na TARURA pamoja na mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji DMDP, masoko ya kisasa na pamoja na ununuzi wa magari matano wamepokea ya takataka yatakayotumika kubeba taka katika sehemu mbalimbali za Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.
Pia alisema shilingi milioni 500 wametengwa kwa ajili ya vituo vya Polisi na milioni 500 kwa ajili ya CCTV kamera kwa sasa kumekuepo na mshikamano mkubwa kati ya chama cha Mapinduzi CCM na Serikali pamoja na Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.
No comments