WAZIRI MAJALIWA ASHIRIKI IBADA YA KUAGA MWILI WA ALIYEWAHI KUWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI FREDERICK WEREMA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, akizungumza wakati wa kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu Mhe. Frederick Werema kwenye ibada iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akitoa salaam za Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa ibada ya kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Frederick Werema iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza Johari akitoa salaam za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa ibada ya kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Frederick Werema iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waombolezaji waliofika kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Frederick Werema wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kwenye ibada iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
No comments