MAKADA WA CCM KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA KATIBU CCM KILOLO
Watu watano akiwemo Boniphace Yohana Ugwale katili wamefikishwa Mahakamani leo kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa katibu wa Chama Cha mapinduzi (CCM)wilaya ya Kilolo Christina Nindi Kibiki na kusomewa shitaka hilo la mauaji.
Watuhumiwa hao walifikishwa Mbele ya hakimu mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Iringa Rehema Mayagilo majira ya saa 8 mchana huku Ulinzi ukiwa umeinarishwa katika viwanja hivyo vya Mahakama .
Wakisomewa maelezo ya Kesi hiyo ya Jinai namba 34404 ya mwaka 2024 kosa la mauaji, mwendesha mashitaka upande wa Jamhuri Sauli Makori aliieleza Mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao Kefa John Wales, Silla Johnson Kimwaga, Boniphace Yohana Ugwale katili , Willy Gerald Chikweo na Hedikosi Gwerino Kimwaga kwa pamoja wanatuhumiwa kumuua Christina Kibiki.
Alisema kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo la mauaji Novemba 12 mwaka 2024 katika Kijiji Cha Ugwachanya wilaya ya Iringa Vijijini.
Hata hivyo alisema upelelezi wa Kesi hiyo bado haujakamilika.
Mahakama hiyo imeahirisha Kesi hiyo hadi Januari 7 mwaka huu Kesi hiyo itakapotajwa tena.
Kati ya waliofikishwa Mahakamani hapo yupo mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wa CCM wilaya ya Kilolo Hedikosi Gwerino Kimwaga huku Katili yeye ni diwani (CCM) wa kata ya Nyanzwa wilayani Kilolo
Source Matukio Media
No comments