RC CHALAMILA: DAR- KUZINDUA BIASHARA SAA 24 FEBRUARI 22, 2025
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya kurejea kwa shughuli za Biashara na kuelekea Uzinduzi rasmi wa mpango shughuli za kibiashara kufanyika saa 24, mkutano uliofanyika katika hotel ya johari Rotana jijini Dar es salaam.
Mkuu wa wilaya ya ILALA, Edward Mpogolo akizungumza katika mkutano huo kufatia kurejea kwa shughuli za Biashara na kuelekea Uzinduzi rasmi wa mpango shughuli za kibiashara kufanyika saa 24, mkutano uliofanyika katika hotel ya johari Rotana jijini Dar es salaam
Mwenyekiti wa bodi ya soko la kariakoo, Bi Hawa Ghasia akitoa taarifa juu ya ujenzi wa soko la kariakoo na hatua ilifikiwa kwa waandishi wa habari mkutano uliofanyika katika hotel ya johari Rotana jijini Dar es salaam.
Dar es salaam - Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila ametangaza rasmi kurejea kwa shughuli za biashara saa 24 ambazo zilisitishwa kufatia kuwa wenyeji wa Mkutano wa Nishati wa wakuu wa Nchi za Afrika ambao ulifanyika January 27 na 28.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mapema leo Januari 30, 2025 katika ukumbi wa Hotel ya Johari Rotana, RC Chalamila amesema jiji la Dar es salaam ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kutambua hilo februari 22 mwaka Mkoa huo utazindua rasmi mpango shughuli za kibiashara kufanyika saa 24.
"Jiji la Dar es salaam ni ya kitovu cha biashara februari 22 mwaka huu tutazindua rasmi mpango shughuli za kibiashara kufanyika saa 24 kwa sasa tupo katika mchakato wa kufunga taa za kutosha na maandalizi ya kufunga kamera yanaendelea vizuri kwa ajili ya usalama ambapo ". Alisema Rc Chalamila
Aidha akizungumzia Mkutano wa Nishati wa wakuu wa Nchi za Afrika RC Chalamila amewashukuru na kuwapongeza wananchi wa Mkoa huo kwa ushirikiano mkubwa walioutoa ikiwemo kuimarisha amani, utulivu na usafi hivvyo ameelekeza wilaya zote kuendelea kusimamia suala la usafi ili Mkoa uendelee kuwa kivutio huku akisisitiza kuwa Serikali inakusudia kuanza kutumia usafiri wa treni na majini kuimarisha usafiri ndani ya jiji hilo.
Akizungumzia suala la ujenzi wa soko la Kariakoo Chalamila ambao umefikia asilimia 97 ambapo Rais Dokta Samia Suluhu ametoa zaidi ya bilioni 28 kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo.
Aidha Rc Chalamila akitokea ufafanuzi juu usafirishaji wa bodaboda na bajaji kuingia mjini amesema kwa sasa hazijazuiliwa kuingia katikati ya jiji zuio ilo lilikuwa la siku chache kutokana na ugeni wa marais wa Afrika.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa bodi ya soko la kariakoo, Bi Hawa Ghasia amesema kuanzia januari 31 wanaanza rasmi kuweka majina ya wafanyabiaahara ambao walikuwepo kwenye soko la kariakoo kabla halijaungua ili wasajiliwe na kwamba baada ya hapo watasajili wafanyabiashara wapya na waliokuwa wanadaiwa wanapaswa kulipa madeni yao.
"February 31, 2025 tutaanza rasmi kuweka majina ya wafanyabiaahara ambao walikuwepo kwenye soko la kariakoo kabla halijaungua ili wasajiliwe baadae tutaanza kusajili wafanyabiashara wapya". Alisema Bi. Ghasia
No comments