Breaking News

RAIS DKT. SAMIA MGENI RASMI MASHINDANO YA YA DUNIA YA QURAN

Dar es salaam - Raiswa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye mashindano ya Dunia ya Quran Tukufu mwaka huu,

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Jijini Dar es Salaam Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Walid Omar amesema mashindano hayo kilele chake ni Februari 23, 2025 na yatafanyika katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Aidha, amesema wananchi wote wanakaribishwa kushiriki katika mashindano hayo na hakuna kiingilio chochote.

Mashindano hayo ni moja yakuhifadhi Quran isipotee ambapo mbegu hii imepandwa na watanzania wenyewe na ikachipua itakayowafanya vijana kusimama katika Imani na maadili mema ili kuleta manufaa katika jamii.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi Abdallah H.Ulega amesema mashindano haya ya Tuzo ya Kimataifa ya Quran Tukufu yanajenga jamii Bora kwa Taifa ambayo ina hofu ya Mungu.

"Quran ni amani kwa hiyo watanzania wote tunajivunia kwa kazi hii ya kusisitiza juu ya amani na maadili mema kwa nchi yetu",amesema Waziri Ulega

Aidha amesema mashindano haya yqnajenga jamii njema yenye ubora bila kujali dini yake kuishi kwa amani

No comments