Breaking News

WAZIRI MAJALIWA MGENI RASMI TUZO YA VALENTINE EVE PATRIOTC AWARD 2025

Dar es salaam - Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe. Kasimu Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni katika hafla ya utoaji wa Tuzo ya Valentine Eve Patriots Award 2025 utakaofanyika February 13 katika ukumbi wa Hyatt Regency jijini Dar es salam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mratibu wa Tuzo hizo ambaye pia ni daktari wa maendeleo ya binadamu na mbobevu wa afya bora ya akili, Dokta Mayrose Majinge amesema lengo la kuandaa tuzo hizo ni kuhamasisha uzalendo kwa kukabiliana na mmonyoko wa maadili na kuondoa madhara ya chuki hasi katika jamii nchini.

"Tuzo hizi ni mahususi kuhamasisha uzalendo, kukabiliana na mmonyoko wa maadili pamoja na madhara ya chuki hasi ambazo vimekuwa vikiathiri sana maisha yetu ya kila siku na kuondoa radha ya maisha kwa muda mrefu ili kupata mwafaka ".Alisema Dkt. Mayrose.

Alisema kwa mujibu wa ripoti za wanasaikolojia mbalimbali zinaonyesha kuwa chuki hasi ni ugonjwa wa kuambukiza unaoenea kwa kasi sana ukiharibu na kuleta maafa katika jamii nyingi hivyo zinahitajika jitahada za dhati kuepuka chuki hasi kwa ajili ya usalama wa kiafya na kiuchumi.

Aidha Dkt. Mayrose aliongeza kuwa jitihada za pamoja zinahitajika katika kuhakikisha kuwa tunakomesha mmomonyoko wa maadili na madhara ya chuki hasi kwani sote ni waanga wa jambo hilo hivyo zinahitajika jitihada za pamoja Katika kutokomoza jambo hilo.

Alisema walengwa wa tuzo hizo ni watu mashuhuri kutoka katika makundi.mbalimbali ya kijammii wakiwemo watumishi na wastaafu wa serikali, Sekta Binafsi, viongozi wa dini, vyama vya siasa, taasisi za elimu, kilimo, viwanda na biasha.

Amewataja wengine ni wadau wa sekta ya habari, taasisi za kutetea haki za binadam, maendeleo ya jamii sanaa na michezo.

Tuzo za mwaka huu 2025 zimebeba kaulimbiu "Uzalendo na maadili mema, Unaanza na mimi na wewe" 

No comments