RC CHALAMILA AONGOZA ZOEZI LA KUFANYA USAFI KUELEKEA MAANDALIZI YA UJIO WA MARAIS AFRIKA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila ameshiriki katika zoezi Maalumu la usafi wa Mji pamoja na Vyombo vya Usalama, Viongozi wa Mkoa, Wilaya, Halmashauri na Taasisi za Umma lililofanyika katika Wilaya ya Ilala.
Akiwa katika zoezi Maalumu la Usafi RC Chalamila ametoa Maelekezo *Sita* ya kuzingatia kuelekea Maandalizi ya ujio wa Marais wa Afrika ikiwa ni pamoja na:-
Mosi, Eneo la feri linapaswa kuwa safi ambapo Mhe. Chalamila amesema Soko Hilo kwa muda mrefu limekuwa haliridhishi katika usafi hivyo kama atagundua bado hali ni mbaya tarehe 23- 25 atapafunga na kuwaleta Jeshi, Polisi, Jkt, Zimamoto, Uhamiaji watafanya usafi mpaka pale watakapojifunza wafanyabiashara hao namna ya kufanya biashara na kutunza mazingira.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ameagiza Mchakato wa kumpata Mwekezaji Mkubwa wa Dampo uharakishwe mara Moja ili dampo lipate mwekezaji Mkubwa anayejitambua anayeweza kuzalisha ajira, gesi, na mbolea
Vile vile RC Chalamila ameongeza kuwa Barabara ya feri kwenda hyati, Johari Rotana mpaka stesheni itafungwa *kwa baadhi ya vyombo vya usafiri* na kuelekezwa vipite wapi ili wageni wetu watakapokuwa hapa kusiwe na foleni kubwa
Aidhaa, Mhe. Mkuu wa Mkoa amemuagiza Katibu Tawala kuwasimamia watendaji wote wa maeneo ya kuanzia TPA kuja Temesa kuelekea Jiji kuwa yawe safi
Wakati huo huo RC Chalamila amesisitiza kuwa Barabara zitakazotumiwa na Marais kwa ajili ya mazoezi ziwashwe taa ili vibaba wadogo wadogo waweze kuwa na aibu kutokana na taa zinazowaka
Mwisho Mhe.Chalamila akasisitiza kuwa kibaka wote kuanzia Leo atakayekamatwa apelekwe maabara ili kiwe chombo Cha kufundishia kwa wanafunzi wanaotaka kuja kuwa wezi (watakaojifunza kuwa wizi haustahili katika Jiji la Dar es Salaam)
No comments