Breaking News

JITOKEZENI KUSHIRIKI MARATHON PUGU - MHASHAMU MUSOMBA

Dar ss Salaam - Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam Mhashamu Stephano Musomba ametoa wito kwa jamii kujitokeza kwa wingi na kuhakikisha wanajiandikisha kushiriki Pugu Marathon awamu ya tatu   itakayofanyika Mei 31, 2025 katika viwanja vya Hija Pugu Jimbo kuu la Dar es Salaam.

Akizungumzia na waandishi habari Jijini Dar es salaam katika Ukumbi wa Kardinali Pengo uliopo Kanisa kuu la Mtakatifu Joseph Jimbo Kuu la Dar es Salaam kuelekea Uzinduzi wa Pugu Marathon awamu ya tatu utakuwa wa kipekee kutikana na kuboreshwa zaidi.

Amesema malengo ya Pugu Marathon awamu hii 2025 ni pamoja na kuendeleza kituo cha Hija Pugu pamoja na kujenga Afya ya kila mmoja kupitia mazoezi.

"Kupitia  mbio hizi kutakuwepo na shughuli mbalimbali zikiendelea ikiwemo utoaji wa huduma za Afya na majitoleo ya matendo ya huruma kwa kutoa Damu kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wenye uhitaji wa damu". Alisema Mhashamu Musomba

Alisema msimu huu wa tatu kutakuwa na mbio za umbali wa kilometer 2.5km, 5km, 10km na 21 Km,malengo ya mbio hizo ni pamoja Kuendeleza kitua cha hija Pugu,Kuendeleza shule ya sekondari Pugu kwa kuboresha maktaba na nyumba aliyoishi Hayati Mwalimu Julius Nyerere,Kufanya matendo ya huruma katika hospitali zetu za Mkoa wa Dar es Salaam na Kujenga afya zetu kupitia michezo.

"Mbio hizi ni za msimu wa tatu ambapo msimu wa pili mwaka 2024 tuliweza  kufanikiwa kupata kiasi cha sh.Milion 160 kutoka kwa wakimbiaji na wafadhili mbalimbali" Aliongeza Mhashamu Musomba.

Aidha amesema  gharama ya mbio hizo ni kiasi cha sh. 30,000 kwa mbio zote kwa maana ya umbali wa Kilomita 2.5,5,10 na 21km ambapo washiriki watapatiwa Tshirt ya kukimbilia,Namba ya kukimbilia na pini za kubandikia pamoja na maji na matunda kwa wakimbiaji.

“Ninawaalika waumini na watu wote wenye mema kuendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizi kwani pamoja na kujenga afya pia itasaidia kuendeleza Kituo cha Hija,” amesema.

 

No comments