WARIOBA: JESHI LA POLISI LISIINGIE KATIKA SIASA
Dar es Salaam - Jeshi la Polisi limeaswa kutojiingiza na kujihusisha na masuala ya siasa na badala yake lijikite kufanya kazi yake ya kulinda usalama wa raia na mali zao.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Warioba wakati akitoa tathimini yake ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hii leo amesema jeshi litakapoingia au kuanza kujihusisha na siasa litaleta mgawanyiko mkubwa kwa wananchi.
“Nitoe rai kwa Jeshi la Polisi kujikita katika kufanya kazi yake ya kulinda usalama wa wananchi halipaswi kujiingiza katika siasa, hali itakayopelekea kuwagawa wananchi, “ Alisema Jaji Warioba na kuongeza kuwa
“Katika siku za karibuni jeshi la Polisi limekuwa likitoa matamko ya kisiasa jambo ambalo sio sahihi wakati wanapaswa kulinda Usalama katika jamii na linatakiwa kufanyakazi zake za kawaida la sivyo watajenga uadui na wananchi,”
Pia ameongeza kuwa Vyama vya siasa wanatakiwa kuangalia maslai ya raia kuachana na chuki, uadui viangalie maslai ya Taifa na sio maslai ya chama vyao.
Alisema ukiangalia yaliyotokea katika uchaguzi niwaombe viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakae na viongozi na wenyeviti wa chama waliopita wawashauri jinsi ya kuendeshea uchaguzi.
Ameongeza kuwa Hakuna kitu cha msingi kama amani na mshikamano tatizo hili linatokana na Serikali inatakiwa kuchukua hatua kuepuka matatizo haya yasijitokeze.
No comments