Breaking News

NCAA YAZINDUA KAMPENI KABAMBE YA UTALII KUELEKEA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA

Na Kassim Nyaki, NCAA Arusha - Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) imezindua msimu wa kampeni ya kuhamasisha utalii kwa wananchi kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka yenye kauli mbiu isemayo _MERRY AND WILD, NGORONGORO AWAITS_ ambayo inatarajiwa kuanza tarehe 4 Desemba, 2024 hadi tarehe 4 Januari, 2025.

Akitangaza kampeni hiyo Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia Idara ya huduma za utalii na Masoko Mariam Kobelo ameeleza kuwa katika utekelezaji wa kampeni hiyo NCAA itashirikiana na kampuni ya _Smile Safaris_ ya Jijini Arusha ambayo katika kuratibu safari hiyo imeandaa vifurushi (Packages) katika makundi matatu ili kuwawezesha watanzania wengi kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro. 
Kamishna Kobelo ameeleza kuwa kifurushi cha kwanza kinaitwa *FARU* ambapo gharama yake kwa mtu ni Shilingi 450,000, watakaolipia gharama hiyo watafanya utalii kwa siku mbili (02) hifadhi ya Ngorongoro na gharama hizo zitajumuisha kiingilio, Malazi, Chakula, muongoza watalii, Usafiri na huduma ya picha ambapo watakaolipia kifurushi hicho safari ya Ngorongoro itafanyika tarehe 24-25 Desembaa 2024.

Kifurushi cha Pili kinaitwa *TEMBO* chenye gharama ya Shilingi 130,000 kwa mtu, kifurushi hiki kinahusisha utalii kwa siku moja (01) Day trip Ngorongoro na gharama hizo zitajumuisha kiingilio, Chakula, muongoza watalii, Usafiri na huduma ya picha.

Kifurushi cha tatu kinaitwa *CHUI* chenye gharama ya Shilingi 85,000 kwa mtu na gharama hiyo itajumuisha Usafiri wa basi, kiingilio, Chakula, muongoza watalii na huduma ya picha.
Katika utekelezaji wa Kampeni hiyo NCAA inatumia vikundi mbalimbali vya Sanaa vikiongozwa na vijana wa _Action Rollers Skates_ na Makachu Jumpers ambao watakuwa katika mitaa mbalimbali kwenye mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Zanzibar kuanzia tarehe 4 hadi 16 Desemba, 2024.

Katika utekelezaji wa kampeni ya kuhamasisha utalii, wananchi wote wanakaribishwa kutembelea vivutio vilivyoko katika eneo laa hifadhi ya Ngorongoro na wanaweza kuchagua kifurushi chochote kati ya vitatu vilivyotangazwa kwa kupiga namba za simu 0755 559013 ili kuweka nafasi (booking)

No comments