SERIKALI KUZICHUKULIA HATUA KALI TAASISI ZINAZOTOA MIKOPO YENYE RIBA KUBWA - DKT. NCHEMBA
Dar es salaam - Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu nchemba amezindua Jukwaa la kwanza la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa mwaka 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Jukwaa litakalotumiwa na wadau kujadili fursa na hatua mbalimbali za kuboresha Sekta ya Fedha ikiwa ni pamoja na huduma ujumuishaji na endelevu za kifedha kwa njia ya kidigitali pamoja na kushirikishana namna bora ya kukuza matumizi ya teknolojia na uvumbuzi ili kukuza na kuimarisha Sekta ya Fedha nchini.
Akizungumza katika Hafla hiyo, Mhe. Dkt. Nchemba aliwahimiza wafanyabiashara na Wananchi kwa ujumla kuweka fedha zao Benki na kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania imeelekezwa na Mhe. Rais kutofunga akaunti za wateja wanaowadai kodi, jambo ambalo TRA, wameanza kulitekeleza.
Alisema jukwaa hilo ambalo linawakutanisha wadau mbalimbali kutoka Sekta ya Fedha za Umma na Binafsi wakiwemo mabenki, taasisi za fedha, kampuni za bima, vyama mwavuli vya sekta ya fedha, vyama vya ushirika wa akiba na mikopo, vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha.
Jukwaa hilo limehudhuriwa pia na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Sauda Msemo na Mkurugenzi wa Hifadhi ya Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Festo Fute.
Dkt. Nchemba amesema Wizara ya Fedha, kwa kushirikiana na Taasisi zake itaendelea kuzichukulia hatua kali Taasisi zinazotoa mikopo yenye riba kubwa (mikopo kausha damu) kwa kiwa inatweza utu wa wakopaji wanaonyang'anywa mali zao kwa kushindwa kulipa mikopo waliyokopa kwenye Taasisi hizo
Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, aliipongeza Wizara Fedha kwa kuandaa Jukwaa hilo na kwamba Wizara yake imetambua umuhimu wa masuala ya uchumi na fedha na imeandaa Mtaala Mpya wa Elimu utakao wawezesha wanafunzi kupata elimu ya ujasiriamali pamoja na biashara ili kuwajengea maarifa ya kujikwamua kiuchumi.
No comments