MONDULI WAFIKIWA NA GARI LA ELIMU YA MPIGA KURA KUHUSU UBORESHAJI WA DAFTARI
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi leo tarehe 7 Desemba, 2024 imetoa Elimu ya Mpiga Kura kwa kutumia Gari la Elimu kwenye minada ya Monduli Juu na Makuyuni iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha ili kuhamasisha wananchi wajitokeze wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Uboreshaji wa Daftari utafanyika Mkoani Arusha, Kilimanjaro na mkoani Dodoma kwenye Halmashauri za Wilaya ya Kondoa, Chemba na Mji wa Kondoa kuanzia tarehe 11 hadi 17 Desemba, 2024 ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Pichani ni wakazi wa Makuyuni Wilayani Monduli mkoani Arusha wakipatiwa vipeperushi vyenye ujumbe kuhusu oboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura wakati gari la Elimu ya Mpiga Kura la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi lililipokuwa likitoa elimu katika Mnada wa Makuyuni kuhusu uboreshaji Daftari la kudumu la Mpiga Kura Wilayani humo Disemba 7,2024.
Mkazi wa Makuyuni Wilayani Monduli mkoa wa Arusha aklisoma kipeperushi cha Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kilichokuwa na maelezo kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura.
Maafisa wa Tume wakitoa Elimu kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura.
Watumishi wa Tume nao wakicheza ngoma ya kimaasai
Burudani kutoka kwa wenyeji ambapo walipanda jukwaani na kutoa burudani.
Burudani kutoka kwa wenyeji ambapo walipanda jukwaani na kutoa burudani.
Mkazi wa Monduli Juu akionesha zawadi aliyopewa na Maofisa wa Tume wakati wa utoaji elimu.
Mkazi wa Monduli Juu Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha akisoma kipeperushi.
Wakazi wa Monduli Juu Wilayani Monduli mkoani Arusha wakisikiliza matangazo kutoka katika gari la Elimu ya Mpiga Kura la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi lililokua likitoa elimu ya mpiga kura kuhusu uboreshaji Daftari la kudumu la Mpiga Kura Wilayani humo Disemba 7,2024. Uboreshaji wa Daftari kwa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro pamoja na baadhi ya Halmashauri za Chemba, Kondoa na Kondoa mji mkoani Dodoma unataraji kuanza Disemba 11 hadi 17 mwaka huu.
No comments