Breaking News

WASIRA:WAHITIMU JIENDELEZENI KWA MASLAHI YENU NA TAIFA

Dar es salaam - Mwanasiasa Mkongwe na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Stephen Wasira amewataka wahitimu wa Chuo hicho kutobweteka na Elimu waliyoipata badala yake wajiendeleze zaidi kwa Maslahi yao na Taifa.

Mzee Wasira ameyasema hayo wakati akizungumza katika Mahafali ya 19 yaliyofanyika katika Kampasi ya Kivukoni jijini Dar es Salaam ambapo Wanafunzi 5,015 wametunukiwa vyeti katika kozi mbalimbali, huku akiutaka Uongozi wa Chuo kujitanua zaidi katika programu za umahiri na shahada ili kuiwezesha jamii kupata Elimu Bora inayoendana na Maadili na Uongozi.

Mwenyekiti huyo wa Bodi pia amemkaribisha Mkuu mpya wa Chuo hicho Prof Haruni Mapesa ambaye ameanza kazi rasmi Novemba 9 mwaka 2024 kwa ajili ya kuendeleza majukumu ambayo Prof Shadrack Mwakalila amekuwa akiyafanya kwa miaka kumi chuoni hapo wakati huohuo amempongeza Prof. Mwakalila kwa Uongozi na ushirikiano na Maendeleo aliyoyapatia Chuo hicho.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Prof. Haruni Mapesa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa Mkuu mpya wa Chuo hicho na kusema ataitumia nafasi aliyopewa kwa kusimamia Maendeleo ya chuo ambacho kimebeba historia, maoni na falsafa za Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere

Aliongeza kuwa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kina historia ndefu, ambapo chimbuko lake ni Chuo Cha Kivukoni ambacho lilianzishwa rasmi Julai 29 mwaka 1961, huku akisisitiza kuwa Chuo hicho kina historia ya kuwa kitovu Cha kufundisha Maadili na Uongozi.

Hata hivyo alisema dhima ya chuo ni kujitolea kwa dhati kuendeleza utoaji wa elimu ya kudumu kupitia ufundishaji bora, utafiti, kuwa na mazingira ya kujifunzia ambapo upataji wa maarifa, utafiti na ubunifu, umakini na stadi tumizi zinatekelezwa na kudumisha


No comments