WAKUFUNZI WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU MILIKI BUNIFU
Wakala wa Usajili wa Leseni za Biashara (BRELA) kwa kushirikiana na Shirika la Miliki Ubunifu ‘Duniani World Interllectual Property Organization’ (WIPO) na Shirika la Miliki Buinfu Kanda ya Afrika (ARIPO) pamoja na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) wameendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wakufunzi watakaokuwa na jukumu la kufundisha wadau mbalimbali juu ya umuhimu na faida ya miliki bunifu ili kuleta chachu ya maendeleo.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Godfrey Nyaisa amesema eneo la Miliki na Bunifu ni moja ya changamoto kwa Bara la Afrika hivyo kwa kushirikiana na wadau wengine kutoa elimu ili kuwajengea uwezo na kuchochea ufanisi katika sekta hiyo yenye utajiri mkubwa.
“Bado kuna changamoto kidogo katika eneo hili la ubunifu kutokana na wadau husika kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu miliki bunifu kutokana na wengi wao kuja na bunifu zao zikiwa hazina sifa, zingine zikitakiwa kurekebishwa ili ziwe na sifa stahiki na kuna nyingine kuwa na sifa lakini wahusika hawajui namna ya kuzirasimisha". Alisema Bw. Nyaisa.
Alisema kwa kutambua hilo Brela kwa kushirikiana na ARIPO sambamba na wadau wengine tukaamua kutoa elimu hii ili nao wakafundishe wengine kuhusu Miliki Bunifu
kuleta hivyo kuleta tija stahiki na kuwa chachu kwa maendeleo na kukuza uchumi wa nchi
Aidha bw. Nyaisa aliongeza kuwa WIPO ikiwa ndio msimamizi mkuu wa Miliki Bunifu Duniani na wameona changamoto ya uwepo upungufu wa ufahamu kwa wadau kuhusu maswala ya miliki bunifu hususani katika nchi za dunia ya tatu kupitia mafunzo tutafanya vizuri kupitia miliki bunifu, Afrika na dunia kwa ujumla.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Willam Anangisye amesema mafunzo hayo ya siku nne yatajikita zaidi katika kiwajengea uwezo washiriki kwani dunia ya sasa ni kama kijiji hivyo mafunzo hayo ni umuhimu ili wakaitoe kwa wengine na kuleta tija stahiki.
“Kupitia mafunzo haya washiriki wataenda kufundisha wengine namna bora ya kulinda bunifu zao, kupitia utafiti ambazo tumefanya unainyesha kuwa watu wengi wamekuwa wakifanya tafiti na kuzifungia kabatini, ni wakati tafiti zetu ziwe bidhaa kwa ajili ya biashara,”. Alisema Prof. Anangisye
Awali mwakilishi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA), bwana Mohamed Ali Maalim amesema mafunzo hayo yatawasaidia kwenda kuwafundisha wabunifu katika maeneo yao ili wazitumie kujiletea maendeleo maana miliki bunifu ni mali kama mali nyingine.
“Kupitia Elimu hii tutakayoipata tutakwenda kuitoa hawana elimu ya kutosha kwa wadau wengine zaidi hili kuwasaidia kulinda mali zao na kujipatia fedha hivyo kuwa kichocheo kwao kufanya bunifu nyingi zaidi kwa ajili ya kujitengenezea kipato". Alisema Bw. Ali Maalim
Kwa upande wa mwakilishi kutoka ARIPO, Outle Rapuleng, amesema kupitia ushirikiano wao na Brela pamoja na wadau wengine wameandaa mafunzo hayo katika semina hiyo baada ya kuona kuna changamoto ya uelewa mdogo kwa wabunifu kutoka nchi zinazoendelea hususan Afrika.
“Naamini kupitia elimu hii tuliyoitoa itasaidia kupata wakufunzi wengi ambao watakwenda katika maeneo yao na kusambaza elimu kuhusu miliki bunifu hivyo kusaidia kuongeza uwelewa kwa wajasiriamali na kuleta mafanikio yanayotakiwa kupitia tasnia ya miliki bunifu, “. Alisema Rapuleng.
Washiriki wa Mafunzo hayo wemetoka nchini mbalimbali za Afrika ikiwemo mwenyeji, Tanzania, Kenya, Uganda, Malawi, Namibia, Zambia, Botswana, Rwanda na nyinginezo lengo likiwa kuwapa elimu kuhusu Miliki Bunifu ambayo watakwenda kuwafundisha wadau mbalimbali katika nchi zao.
No comments