CHAMA CHA NLD MGUU SAWA KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
Chama cha National League for Democracy (NLD) kimesema kimejipanga kuhakikisha kuwa kinashinda katika uchaguzi wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji, na vitongoji unaotarajiwa kufanyika badae mwezi huu nchi nzima
Kauli hiyo imetolewa mapema
leo Novemba 5, 2024 na Katibu Mkuu wa Chama cha hicho, Mhe. Doyo Hassan Doyo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Tanga, amesema chama kipo tayari na kimejipanga kihakikisha kuwa kinashinda kwa kishindo katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa, vijiji, na vitongoji unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Mhe. Doyo alisisitiza kuwa chama hicho kimefanya tathmini ya kina na kisayansi kabla ya kushiriki katika uchaguzi na kimejiridhisha kuwa kitafanya vyema katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa, vijiji, na vitongoji Tanzania bara na Zanzibar.
Alisema chama NLD kitasimamisha wagombea wenye siga na ushawishi zaidi ya 600 nchi nzima, ikijumuisha wagombea wa nafasi mbalimbali za ujumbe.
Katika hatua nyingine mhe. Doyo ameipongeza TAMISEMI kwa maandalizi mazuri ikiwa ni pamoja na kuwepo na ushirikishwaji wa wadau katika hatua zote tangu kuanza kwa zoezi hilo nchini.
Alisema pia kumekuwepo na uwazi katika kipindi chote cha zoezi hilo pamoja na usimamizi bora kuanzia ngazi ya undikishaji na urejeshaji wa fomu.
"Wote ni mashahidi mwaka huu zoezi limeenda vizuri na kufanyika kwa uwazi tangu hatua ya awali ikilinganishwa na chaguzi zilizopita". Alisema Mhe. Doyo.
Aidha Doyo amesisitiza umuhimu wa utekelezaji wa "4R" za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha demokrasia, huku alisisitiza kuwa ameziona "4R" za Mhe. Rais, kwa vitendo katika maandalizi ya uchaguzi huu wa serikali za mitaa, vijiji, na vitongoji.
"Chama kimejipanga na kina matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji utakaofanyika Novemba 27, 2024 nchi nzima kutokana na maandalizi tuliyofanya". Alisema Mhe Doyo
No comments