Breaking News

TAMISEMI YAWAPIGA MSASA WAANDISHI WA MTANDAONI KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITA

Ofisi ya Rais tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) imeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa waandishi wa habari za kimtandao (JUMIKITA) ili kuwaongezea weledi na kuzifahamu kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27. 2024 

Akizungumza katika Ufunguzi wa mafunzo hayo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) anayeshugulikia Afya Dkt Grace Magembe amesema lengo la kuwapatia mafunzo hayo ni kutambua umuhimu wao wa kutoa taarifa kwa jamii kupitia mitandao ya kijamii na kuwafikia watu wengi katika mda mfupi.

"Tunatambua nyinyi ni kundi kubwa na Serikali inatakiwa iwatambue ndio maana tumeaandaa mafunzo, nichukue nafasi hii kuwapongeza hii kazi mmeshaianza ila hapa tunajengeana tu uwezo ili muifanye vizuri zaidi ,hizi kanuni sio kila mtu ana elewa watu wasipoelewa inakuwa ni chanzo cha malalamiko". Alisema Bi.Magembe

Aidha bi Magembe aliongeza kuwa mafunzo hayo kuwajengea uwezo waandishi wa Kidigitali itapelekea wao kupelekea taarifa za uhakika na weledi ili uchaguzi ufanyike kwa amani na uhuru

Uchaguzi wa Serikali za mitaa na vijiji unatarajiwa kufanyia nchi nzima 27 novemba 2024 

No comments