Breaking News

WATU MILIONI 300 AFRIKA KUTUMIA NISHATII YA UMEME IFIKAPO 2030 - DKT. BITEKO

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt. Doto Biteko amesema ifikapo mwaka 2030 watu milioni 300 katika Bara la Afrika watakuwa wanatumia Nishati ya umeme.

Amesema  juhudi zinazofanyika katika kufikia lengo hilo zimepelekea  Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Benki ya Dunia ( WB) kuunga mkono Tanzania katika miradi mbalimbali ikiwemo Ajenda ya Nishati Safi ya kupikia.
Biteko amesema hayo wakati akizungumza katika Mkutano wa Jukwaa la Majadiliano kuhusu Masuala ya Nishati  kwa Bara la Afrika kwa ngazi ya Mawaziri unaofanyika Jijini Dar es salaam kwa siku mbili ulioandaliwa  na Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na AfDB. 

Amesema AfDB imeichagua Tanzania kufanya mkutano huo wa majadiliano kwa kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa kimaendeleo na mafanikio katika Sekta ya Nishati ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika zinazoshirikiana na benki hiyo na imekuwa mfano wa kuigwa na nchi hizo..


No comments