Breaking News

DKT MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NGORONGORO ONYESHO LA KIMATAIFA LA SWAHILI EXPO (S!TE)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi akipata maelezo kuhusu shughuli za Uhifadhi, vivutio vya utalii mubashara kutoka eneo la hifadhi ya Ngorongoro na fursa za uwekezaji zilizopo hifadhi ya Ngorongoro kutoka kwa Meneja wa Huduma za Utalii na Masoko NCAA Mariam Kobelo (kushoto) wakati wa Ufunguzi wa Onesho la Kimataifa la Swahili International Tourism EXPO (SITE) linalofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Kulia kwa Rais Mwinyi ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) na kushoto kwa Rais ni Naibu katibu Mkuu (Utalii) Nkoba Mabula.

Mamlaka ya Hifadhi ya Hifadhi ya Ngorongoro ni moja kati ya Taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii zinazoshiriki onesho hilo lililoanza tarehe 11- 13 Oktoba, 2024.

No comments