Breaking News

ATLAS SCHOOLS HALF MARATHON 2024 KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUBORESHA USALAMA WA MTOTO

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Siku ya Atlas (Atlas Day 2024) Mwalimu Willbroad Prosper akifafanua jambo kuhusu Atlas Schools Half Marathon, Mahafali, Maonyesho na michezo ya watoto itafanyika Oktoba 14 katika viwanja vya shule ya Atlas Madale.

Dar es salaam:
Shule za Atlas Primary School na Sekondary umeandaa ATLAS DAY 2024 ambayo itakuwa na lengo la kuungana na Serikali kuboresha usalama wa watoto na pia kutokomeza ukatili dhidi ya watoto.

Akizungumza jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Siku ya Atlas (Atlas Day) Mwalimu Willbroad Prosper amesema siku hiyo ambayo mahususi inatajumuisha Atlas Schools Half Marathon, Mahafali, Maonyesho ya vitu mbalimbali pamoja na michezo ya watoto na burudani ambayo itafanyika Oktoba 14, 2024 katika viwanja vya Atlas Schools Madale.

"Siku hiyo ya oktoba 14 kuanzia saa 11:00 Alfajiri kutakuwa na mbio yaani Atlas Schools Half Marathon ambapo tutakua na mbio za 21km, 10km na 5km na baadae kufuatiwa na Mahafali pamoja na matukio mbalimbali". Alisema Mwalimu Prosper.

Alisema mbio Atlas Schools Half Marathon 2024 ambazo Lengo kuu la kuwa na mbio hizi kwa mwaka huu ni kuungana na Serikali kuboresha usalama wa watoto na pia kutokomeza ukatili dhidi ya watoto, ambapo mwaka huu zimebeba kaulimbiu ya "Run for Wellness, Good health for our future generation” zitaanzia hapa hapa katika viwanja vya shule za Atlas Madale na kuhitimishwa hapa hapa (Yaani starting na Finishing Point ni hapa hapa shuleni),

Mwalimu Prosper alibainisha kuwa mwaka huu tarehe ya kufanyika kwa mbio yetu imeangukia siku ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl. JK Nyerere tarehe 14/10/2024 na kama ilivyo ada kwa miaka ya nyuma basi tutakua tukisherehekea kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere kwa kuenzi kazi nzuri alizozifanya katika Taifa katika kipindi cha uhai wake.

"Kwa wale wote watakaopenda kushiriki mbio 5km, 10km na 21km Tshs 35,000 kwa mtu mmoja, kwa kikundi cha watu wasiopungua 20 watapata punguzo la asilimia 10 Tshs 31,500, ambapo mshiriki atapata Fulana, Namba ya kukimbilia (bib number), na njiani atapata huduma zoote muhimu za kukimbia kama vile Maji, Matunda, huduma ya kwanza, wrist band, na medali na viburudisho kama vile soup yenye viwango na nyama choma," Alisema Mwalimu Prosper.

Alisema usajili wa washiriki wa mbio hiyo unaendelea katika Shule zote za Atlas, yaani Atlas Primary School na secondary Madale, Atlas Primary School Ubungo na pia Mlimani City ua kupitia Lipa namba Tigo 5927380 Atlas Schools. ambapo ukisha sajili tu utapatiwa vifaa vyako cha kukimbilia siku ya Oktoba 14, 2024, 

Aidha mwalimu Prosper aliongeza kuwa mara baada ya marathon itafatiwa na Mahafali ya 19 ya shule za Atlas ambapo wanafuzi zaidi ya 700 wa Nursery, Darasa la Saba na Kidato cha nne kutunukiwa VYETI vya kuhitimu kutoka katika shule zote tatu Atlas Primary School Ubungo, Atlas Primary School na Secondary School Madale.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Riadha (RT) Mkoa wa Dar es Salaam Samwel Mwera ameshukuru kwa namna Shule za Atlas zinavyoandaa mbio hizo kwani wamekuwa wakishirikiana hatua kwa hatua na kwamba uongozi wa shule umekuwa ukifuata taratibu zote.
Awali Mjumbe wa Kamati ya Ufundi kutoka Mamlaka za Usajili Riadha Ranzania (RT) Kanda ya Pwani Felix Chunga amesema kwamba Shule za Atlas zimekuwa ni mdau wao mkubwa na wamekuwa wakishitrikiana kwa msimu wa tano sasa.

"Ni wajibu watu kuhakikisha tunasimamia mbio hizo hili kuhakikisha kuwa zinafuata taratibu na sheria, hivyo tumekuwa tukishirikiana na Shule za Atlas kuboresha mbio hizo hili kuendelea kuwa Bora karibu kila mwaka". Alisema Bw. Chunga

No comments