Breaking News

HANSPAUL GROUP TUNAIUNGA MKONO SERIKALI MATUMIZI YA NISHATI SAFI

Kampuni ya Hanspaul Group ambayo Imebobea katika utengenezaji wa magari ya kubebea watalii imesema kuwa imejipanga kwa kuhakikisha kuwa inazalisha magari yatumia teknolojia ya Nishati ya Umeme kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan matumizi ya nishati safi.

Akizungumza katika. Mahojiano na mwandishi wa wa mtandao huu katika ufunguzi wa Onyesho nane la kimataifa ya utalii (S!TE EXPRO 2024) jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji Kampuni hiyo, bwana Satbir Singh Hanspaul amesema kama Kampuni tunatambua na kuona jitiha hizo zinazofanywa na serikali hiyo kuunga mkono kwa kutumia teknolojia ya nishati ya umeme katika magari yao.

"Kampuni yetu tayari imeshachukua hatua ya kuiunga mkono Serikali yetu, kwa kutumia nishati safi kwani Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Wizara ya Utalii wameshaonyesha dhamira ya dhati hususani kwa kuweka Mazingira wezeshi na mifumo Mzuri". Alisema Bw. Hanspaul.

Alisema Serikali tayali imeweka na kuandaa Mazingira rafiki hususani kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi jambo lililosaidia kampuni yetu kutengeneza teknolojia mpya ya matumizi ya nishati ya Umeme katika magari ya Utalii, kwa lengo la kuwezesha kuwa na Utalii wa kijani (Green Tourism).
Tanzania imekuwa ikisifiwa kote duniani kwa kuwa na amani jambo linalopelekea kuvutia watalii wengi kutoka mataifa mbalimbali kuja kutembelea hifadhi zetu kwani hakuna Utalii bila amani hivi vitu ni lazima viende pamoja, tupo tayari kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Aidha katika hatua nyingine Bw. Hanspaul aliongeza kuwa Kampuni tayali imeshafungua tawi Mkoani Arusha na Tumefanikiwa Kuuza magari haya katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Namibi na Ethiopia na bado tumejipamga kuendelea kutafuta masoko katika nchi zingine barani Afrika.

Katika hatua nyingine akizungumzia ubora wa magari hayo bwana Hanspaul amesema magari hayo yameifanya Tanzania kuwa moja ya nchi ambazo zinajari mazingira na kupitia bidhaa hiyo inaifanya Tanzania kuwa katika soko la juu.

"Utalii ni moja ya kipaumbele kwa Nchi yetu, ni moja sekta inayoingiza fedha nyingi za kigeni hivyo Kampuni yetu tumeamua kutumia bidhaa hii ya green tourism ili kuisaidia serikali kutekeleza adhma yake ya kutumia Nishati safi na salama ili kuhifadhi Mazingira.

No comments