Breaking News

WMA: YAJIPANGA KUONGEZA MAPATO KATIKA MFUKO MKUU WA SERIKALI HADI BILIONI 7 MWAKA UJAO WA FEDHA

Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA), Bw. Alban M. Kihulla, akitoa wasilisho lake mbele ya Wahariri wa vyombo vya Habari Septemba 11, 2024 jijini Dar es salaam

Mwakilishi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Sabato Kosuri
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bw. Deodatus Balile (kulia) na baadhi ya maafisa wa WMA

Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA), Bw. Alban Kihulla (kulia) akiwa na mwakilishi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Sabato Kosuri, akionesha tuzo ambayo WMA walitunukiwa kwa kuwa taasisi bora ya umma kuwasilisha Gawio kwa wakati.
Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA), Bw. Alban Kihulla (wapili kushoto), akiwaeleza Wahariri na Waandishi wa habari, matumizi ya 50 vipimo mbalimbali

Na Khalfan Said: Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) imepania kuongeza mchango wake katika mfuko mkuu wa Serikali hadi kufikia shilingi bilioni 7.7 mwaka 2023/2024, Mtendaji Mkuu wa WMA, Bw. Alban Kihulla, amesema.


Bw. Kihulla ameyasema hayo jijini Dar Es Salaam, wakati akitoa wasilisho lake kuelezea mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya wakala wa vipimo kwa wahariri  wa vyombo vya habari Septemba 11, 2024.

Amesema, Juni 11, 2024 kati ya taasisi 258 za Umma, WMA ilipata tuzo kama taasisi bora inayochangia kwa wakati katika mfuko mkuu wa serikali, ambapo katika mwaka wa fedha 2022/2023 taasisi hiyo ilitoa Gawio la shilingi bilioni 4.3

“Tunafanya hivi kwa sababu ni lazima tuangalie mipango ya maendeleo ya nchi inakwenda na hivyo WMA inaowajibu wa kuchangia ili kuiwezesha serikali kutekeleza mipango iliyojiwekea kwa wakati.” Amefafanua.

Akizungumzia majukumu ya WMA, Bw. Kihulla amesema inahusika sio tu na mizani za kupima uzito bali inahusika na Vipimo kwa ujumla wake na majukumu yake ni pamoja na kumlinda mlaji katika Sekta ya Biashara, Usalama, Mazingira na Afya kupitia matumizi ya vipimo sahihi.

Lakini pia, Kuilinda jamii kuepukana na madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya vipimo katika Sekta ya Biashara, Usalama, Mazingira na Afya,

Aidha WMA pia inaowajibu wa kusimamia na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wanaojihusisha na utengenezaji, uundaji, na uingizaji wa vipimo mbalimbali katika Biashara, Usalama, Mazingira na Afya ili kuwa kiungo kati ya taifa na taasisi za kikanda na Kimataifa katika masuala ya Vipimo (Legal Metrology).

Majukumu mengine ametaja kuwa ni kuhakikisha vifaa vyote vitumikavyo nchini kama standards za vipimo vinaulinganisho sahihi na ule wa Kimataifa, Kukagua na kuhakiki bidhaa zilizofungashwa (Net quantity & labeling) na kutoa elimu na ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya vipimo kwa wadau.

No comments