Breaking News

WATOA HUDUMA ZA UTALII ZAIDI YA 120 KUSHIRIKI SWAHILI INTERNATIONAL EXPO SITE 2024

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), bwana Ephraim Mafuru akifafanua jambo kuhusu maandalizi ya onesho la Nane la Swahili International Tourism Expo SITE 2024 litakalofanyika Oktoba 11 hadi 13 katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam
Washiriki zaidi ya 120 kutoka Nchi takribani 120 ambazo ni masoko ya kimkakati ya utalii wa Tanzania ikiwemo Nchi za Asia, Ulaya, na Amerika wanatarajiwa kushiriki katika Onyesho Nane la Swahili International Tourism Expo SITE 2024 linalotarajiwa kufanyika Oktoba 11 hadi 13 katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es salaam juu ya maandalizi ya onyesho hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), bwana Ephraim Mafuru amesema mwaka huu jumla ya waonesha wa bidhaa (Exhibitors) na huduma za utalii zaidi ya 120 sambamba na wanunuzi wa bidhaa na huduma za utalii (International Hosted Buyers) wamedhibitisha kushiriki. 

"Kwa mwaka huu Onesho la S!TE 2024 washiriki mbalimbali wamedhibitisha ikiwa ni pamoja na Wakala wa Biashara za Utalii (Tour Operators), Watoa Huduma za Malazi (Accommodation Facilities), Wakala wa Safari (Travel Agents), Wakala wa Meli za Watalii (Cruise ship agents)na Waongoza Watalii (Tour Guides)," Alisema Bw
Mafuru. 

Alisema Vyama vya Utalii (Tourism Associations), Wajasiriamali wa bidhaa za utalii, Bodi za Utalii (Tourism Boards), Taasisi za Uhifadhi (Conservation Authorities), Taasisi za Kifedha (Financial Institutions) na Taasisi za Elimu za Utalii (Tourism Learning Institutions).  

Aidha bwana Mafuru aliongeza kuwa shughuli mbalimbali zitafanyika matika Maonyesho ya S!TE 2024 ikiwemo Maonesho ya Utalii (Exhibitions), Mikutano ya Kibiashara (B2B, B2G, B2C, G2G), Semina za masuala ya utalii na masoko (Seminars), Jukwaa la Uwekezaji katika Sekta ya Utalii (Tourism Investment Forum) na Ziara za Mafunzo za kutembelea vivutio vya utalii (FAM Trips). 

Amesisitiza kuwa ziara hizo zitajikita katika Kanda za Utalii Kusini (Southern Circuit), Magharibi (Western Circuit) na Zanzibar kama Gombe National Park and Kigoma City Tour, Mikumi and Udzungwa Mountain National Parks, Ruaha National Park and Iringa Active Safari Fam Trip, Nyerere National Park, Pugu Kazimzumbwi Forest, Dar es Salaam and Kilwa Ruins, Mafia Island, na Zanzibar Fam Trip.

Onyesho la S!TE 2024 mwaka huu limebeba Kauli Mbiu ya S!TE 2024: “Explore Tanzania for a Life Time Investment and Seamless Tourism Experience” au “Tembelea Tanzania kwa Uwekezaji Endelevu na Utalii usiomithirika”. 

Nchi zilizothibitisha kushiriki Onyesho la S!TE 2024 China, Denmark, Finland, Japan, Afrika Kusini, Hispania, India, Oman, Urusi, Misri, Uholanzi, Nigeria, Brazil, Ujerumani, Kenya, Ethiopia, Uganda, Lesotho na wenyeji Tanzania

No comments