Breaking News

SWAHILI INTERNATIONAL TOURISM EXPRO "S!TE 2024" KUFANYIKA OCTOBA 12 - 13 JIJINI DAR

Mkurugenzi Mkuu bodi ya Utalii Tanzania Bw. Ephraim Mafuru akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya maandalizi ya onesho la Swahili International Tourism Expo (S!TE2024) litakalofanyika Oktoba 11 Hadi 13, 2024 katika ukumbi wa mlimani City Jijini Dar es Salaam

Dar es Salaam:
Serikali imesema itaendelea kukuza sekta ya utalii kwa kuvitangaza kimataifa vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imetarajia kufanya onesho la  nane la Swahili International Tourism Expo ( S!TE) Oktoba 11 Hadi 13, 2024 katika ukumbi wa mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bwana Ephraim Mafuru amesema onesho hilo la kimataifa litakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya utalii nchini.

Alisema lengo la kufanya onyesho hilo ni kuwakutanisha Watoa huduma waliopo katika mnyororo wa thamani wa Utalii Ndani na nje ya Nchi ambao pia watapata fursa ya kuonesha bidhaa zao za Utalii na kutengeneza Mtandao wa Biashara (Business Network)

"Maonyesho la S!TE 2024 linaenda sambamba na Utekelezaji wa sera ya Taifa ya Utalii ya Mwaka 1999 pamoja na mkakati wa kutangaza Utalii Kimataifa ( 2020-2025 ) ambayo imetilia mkazo kutangaza Tanzania kama kivutiok Bora Cha Utalii Duniani". Alisema Bw Mafuru.

Bw. Mafuru aliongeza kuwa kipitia Onyesho hilo ambalo pia ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka mitano ambapo zao la Utalii wa Mikutano na Matukio (MICE Tourism) limeanishwa kama zao la Utalii la kimkakati kwa lengo la kufikia watalii milioni tano na mapato ya Dola za Marekani bilioni sita ifikapo Mwaka 2025.

"Manyesho ya nane ya S!TE 2024 yamebeba ujumbe usemao "Explore Tanzania for a Life Time Investment and Seamless Tourism Experience" ambapo onesho hilo litahudhiliwa na waoneshaji wa bidhaa na huduma za Utalii zaidi ya 120 sambamba na wanunuzi wa bidhaa na huduma za Utalii (International Hostel Buyers) taktibani 120.

Amezitaja nchi hizo ambazo ni masoko ya Kimkakati ya Utalii wetu ikiwemo Ulaya, Asia na Amerika

Pia katika Maonyesho ya S!TE 2024 kutakuwa na ziara za mafunzo ((FAM trips) ambazo zinalenga kuwajengea uelewa wahudumu wa bidhaa za Utalii kuhusu vivutio vya Utalii vilivyopo Tanzania ili waweze kuvitangaza katika Nchi zao na dunia kwa ujumla.

"Mwaka huu ziara hizo zimejikita katika kufungua Kanda za Utalii zinazochipukia ikiwemo ukanda wa Utalii Magharibi ( Western Circuit) na Ukanda wa Utalii Kusaini (Southern Circuit) na kufunganisha shughuli za Utalii zinazofanyika Zanzibar na Tanzania Bara." Alisema Bw. Mafuru.

No comments