Breaking News

SERIKALI IKO MAKINI KUDHIBITI CHANGAMOTO ZA WANYAMAPORI WAKALI - MHE.CHANA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana kifafanua jambo wakati akizungumza katika Semina ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Songea, Mkoani Ruvuma.
Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda akiongea katika Semina ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Songea, Mkoani Ruvuma.

Ruvuma
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Balozi, Dkt. Pindi Chana amesema Serikali imejidhatiti katika utatuzi wa changamoto ya migongano kati ya wanyamapori na binadamu chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ameyasema hayo leo Septemba 27, 2024 katika Semina ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Songea, Mkoani Ruvuma. 

"Mojawapo ya mikakati ya Serikali katika kutatua changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu nimetoa kibali kwa baadhi ya maeneo yenye changamoto tutavuna mamba, viboko na tembo kupitia uwindaji wa kitalii" amesisitiza Mhe. Chana.

Aidha, amesema Serikali inatumia ndege nyuki (drones) kufukuza tembo, kujenga vituo vya askari uhifadhi na kufunga tembo viongozi kola kuzuia wasiingilie katika makazi ya watu.

Semina hiyo imehudhuriwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ikiongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda.



No comments