Breaking News

NATASHA "TUWAENZI NA WASANII WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI"

Msanii wa Maigizo  Suzana Lewis maarufu kama (Natasha) ameungana na wasanii wengine leo  Septemba 7, 2024 katika Dua maalum  ya kuwakumbuka  wasanii waliotangulia mbele ya haki.

Akizungumza mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Leaders ambapo yanafanyia maadhimisho hayo amesema wasanii wote waliotangulia mbele ya haki wameacha mapengo mengi ambayo hayawezo kuzibika.

“Tutaendelea kuwakumbuka na kuwaenzi kwa kazi zao walizozifanya kwani kuwaenzi ni jambo kubwa sana kutokanana kazi kubwa ya sanaa walizofanya,”. Alisema Bi. Natasha.
Amesema Kuna watu wameondoka wakiwa wadogo sana  na wengine wakubwa tulikuwa nao karibu lakini wameacha pengo kubwa sana.

Amewataja baadhi ya wasanii hao ambao baadhi alifanikiwa kufanya kazi nao katika kipindi cha uhai wao kuwa ni pamoja na Kanumba, Maunda Zolo na  Amina Chifupa ambaye alikuwa rafiki yake mkubwa.


No comments