Breaking News

MAONESHO YA KIMATAIFA YA VIWANDA (TIMEXPO) 2024 KUANZA SEPTMBA 26 HADI OKTOBA 2

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI) wameandaa maonesho ya Kimataifa ya  viwanda maarufu kama TIMEXPO ambayo yatafanyika tarehe 26 Septemba, hadi tarehe 2 Oktoba 2024 katika Kiwanja cha JK Nyerere (Sabasaba) kilichopo katika Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Bw. Tito Nombo ambaye  amemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Bi Latifa Khamis ameeleza kuwa  TanTrade Pamoja na majukumu mengine ina jukumu la kusimamia maonesho ya kisekta ikiwa ni Pamoja na Maonesho ya Viwanda ambapo ni fursa kubwa kwa wenye viwanda vidogo , vya kati na vikubwa kushiriki ili kubadilishana uwezo katika teknolojia, ubunifu, uzoefu na kupata masoko kwa kuwa maonesho haya yatahudhuriwa na wenye viwanda kutoka nje ya nchi wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika leo tarehe 2 Septemba, 2024 katika

No comments