Breaking News

TANZANIA NA JAPANI KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ( TanTrade)  Bi. Latifa M. Khamis amepokea ujumbe kutoka benki ya ushirikiano wa Kimataifa kutoka Japani kushirikiana na TanTrade ili kuongeza wigo wa makampuni kutoka Japani kushiriki katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam pamoja na uwekezaji katika eneo la kiwanja cha maonesho ya Sabasaba ambapo ni eneo lenye tija na thamani  katika ukuzaji wa uchumi nchini  Tanzania wakati wa kikao kifupi kilichohusu mahusianao ya kibiashara kati ya Tanzania na nchi ya Japani  kilichofanyika  leo tarehe 3 Septemba, 2024 katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi za Tantrade zilizopo barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Aidha Mkurugenzi wa Benki ya ushirikiano wa Kimataifa Bw. Shinya Yoshida ameahidi kuendelea kuunga mkono maendeleo ya biashara na uwekezaji ndani ya Tanzania pamoja na nchi ya Japani  ikiwa ni kuhakikisha bidhaa za Kitanzania zinapata masoko Japani


No comments