Breaking News

CHEMBA YA BIASHARA YA DUBAI YATUA TANZANIA

Chemba ya Biashara ya Dubai leo tarehe 3 Septemba 2024 imetembelea Makao Makuu ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu Bi Latifa M. Khamis, huku lengo la ujio wao likiwa ni kujadili namna taasisi hizi mbili zinaweza kushirikiana kwenye maeneo mbalimbali katika Sekta ya Biashara pamoja na namna TanTrade wanaweza shirikiana na Chemba katika kufanikisha Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Dubai linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam, mwezi Octoba 2024.

Aidha Bi. Latifa amewahakikishia Chemba ya Biashara ya Dubai kuwa TanTrade itahakikisha kuwa inawaunganisha na wadau walengwa na itashirikiana nao kikamilifu katika uratibu wa kongamano.




No comments