Breaking News

MAFIA BOXING PROMOTION YAJA NA PAMBANO LA USIKU WA KIHISTORIA "KNOCKOUT YA MAMA" KUFANYIKA OKTOBA 5, DAR

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mafia Boxing Promotion, bwana Antonio Nugaz akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya pambano kubwa la kimataifa la ngumi "Knockout ya Mama" Uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa City Center Hall jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam
Kampuni ya Mafia Boxing Promotion imetangaza rasmi kufanya pambano la kubwa la ngumi la Kimataifa lilopewa jina la "Knockout ya Mama" litakalofanyika Oktoba 5, 2024 katika ukumbi wa City Centre Magomeni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza juu ya maandalizi ya pambano Hilo jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo bwana Antonio Nugaz amesema pambano hilo litawakutanisha mabondia Ibrahim Mafia Tz na Said Chino katika kuwania mkanda wa WBC.

“Mara nyingi katika Mchezo wa Mpira wa miguu, Rais Dkt Samia amekua akitoa zawadi ya fedha kwa kila Gori linalofungwa katika mechi za Kimataifa ili kuleta motisha kwa wachezaji, nasisi huku atujakaa mbali tumeamua kuja na pambano hili (Nock out ya Mama) mshindi atapata milioni kumi kama bonasi”. Alisema Bw. Nugaz.

Alisema pambano hilo la Kimataifa limelenga zaidi kuongeza hali kwa mabondia wa kitanzania kupigana zaidi Kimataifa ili kufikia Malengo yao.

Aidha bwana Nugaz laiongeza kuwa kwa kutambua hadho ya pambano Hilo wamepanga kuwa na mgeni rasmi ambaye atatangazwa hivi karibuni.

Alisema katika kuhakikisha kuwa wapenzi na mashabiki wa mchezo huo wanapata burudani na kushuhudia pambano Hilo ambalo limeandaliwa kwa viwango vya kimataifa tayali wakate tiketi katika maeneo mbalimbali ambapo ametaja viingilio kuwa ni elfu kumi 10,000, 30,000 na 50,000.
Kwa upande wake bondia Ibrahim Mafia Tz na Said Chino wakizungumzia maandalizi kuelekea pambano Hilo wamesema hao wapo tayari kupambana katika pambano hilo hivyo tutoe Rai kwa wapenzi na mashabiki wa mchezo wa ngumi kujitokeza kwa wingi siku hiyo kupata burudani ya aina yake.

“Tumejiandaa vizuri kazi itaonekana naamini hivo, mashabiki watapata burudani ya kutosha na pia nitashinda pambano hilo” Walisema mabondia hao wakati wakizungumzia na mwaandishi wa mtandao huu









No comments