Breaking News

KATIBU MKUU WA CHAMA CHA NLD DOYO HASSAN DOYO SEPT 11 RASMI AANZA ZIARA YA UJENZI WA CHAMA ZANZIBAR

Katibu Mkuu wa cha National League for Democracy (NLD), Mhe. Doyo Hassan Doyo, akiwasili zanzibar leo tarehe Septemba 11, 2024 kuanza rasmi ziara ya Ujenzi wa chama pamoja na kujitambulisha kwa wanachama.
 
Zanzibar
Katibu Mkuu wa cha National League for Democracy (NLD), Mhe. Doyo Hassan Doyo, leo tarehe 11-09-2024 amewasili Visiwani Zanzibar kwa ziara ya chama cha NLD. Katika ziara hiyo, Mhe. Doyo ameambatana na viongozi mbalimbali wa chama hicho kutoka upande wa Bara na kupokelewa na baadhi ya viongozi wa chama hicho upande wa Zanzibar, akiwemo Mwenyekiti wa chama cha NLD Taifa, Mhe. Mfaume Khamis Hassan.

Mhe. Doyo na Mwenyekiti wa NLD walifanya kikao cha ndani na baadhi ya wanachama wa chama hicho upande wa Zanzibar, ambapo wote kwa pamoja walitoa mwito wa kuimarisha ujenzi wa chama na ushirikiano kati ya wanachama wa NLD kutoka Bara na Zanzibar.
Akizungumza na wanachama wa NLD mara baada ya kuwasili Mwenyekiti wa chama hicho Mhe. Mfaume Khamis Hassan aliwataka wanachama wa NLD nchini kumuunga mkono Mhe. Doyo ili kuleta mabadiliko ndani ya chama hicho, akimwelezea Mhe.Doyo kama mtu muadilifu na mtendaji mzuri wa kazi za chama.

"Kutokana na mchango wake mkubwa katika siasa nchini Hakuna chama chochote cha chenye malengo chanya kinachoweza kumkataa mtu kama Doyo, mtu mwenye historia ya utendaji bora katika siasa za nchi hii.".  Alisema Mhe. Hassan. 
Kwa upande wake, Mhe. Doyo aliwashukuru wanachama wa NLD kwa utayari wao wa kufanya kazi naye, na akawahakikishia kwamba atafanya mabadiliko makubwa katika ndani ya muda mfupi hasa katika kipindi hiki tukiwa tunaelekea katika uchaguzi za serikali za mitaa  mwezi Novemba na uchaguzi mkuu ujao mwaka 2025 

Alisema Katika kuhakikisha chama kinakuwa na kuwa chama shindano nchini niko tayari kupokea baadhi ya wanachama wanaoniunga mkono kutoka sehemu mbalimbali nchini katika harakati za muendelezo wa kuimarisha demokrasia.

"Nyuma yangu kuna kundi kubwa wanachama wapya linalofurahishwa na sera nzuri za chama cha NLD hasa inayosisitiza uzalendo, haki, na maendeleo kwa umma,". Alisema Mhe Doyo
Alisema nikuahidi Mwenyekiti na wanachama wote kuwa chama kinaenda kuwa miongoni mwa vyama shindani katika chaguzi zijazo. na ukombozi wa umma utakuja chini ya mwamvuli wa NLD.

Kesho, Septemba 12, 2024 viongozi wa chama hicho wataendelea na ziara yao ya ujenzi wa chama katika jimbo la Chaani.




No comments