Breaking News

KANISAA ANGLIKANA LA EPISCOPAL TANZANIA KUIUNGA MKONO SERIKALI KATIKA SEKTA YA AFYA, MAJI NA MICHEZO

Tangu Uhuru mpaka hivi Sasa Taasisi za dini zimekuwa na mchango mkubwa Sana Nchini katika kisisimua maendeleo na kusimamia maadili katika Jamii ya Kitanzania 

Ni vema na haki tukawaunga mkono, Kama Kanisa la Anglikan la Episcopal Tanzania linaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Miradi ya Maji Vijijini ,Sekta ya Elimu kujenga madarasa na shule , kujenga Zahanati kwenye Sekta ya Afya , 

Ameahidi Askofu Mkuu Elibariki Philip KUTTA kujenga uwanja mkubwa wa kisasa wa michezo wilayani Kongwa mkoani Dodoma kuunga mkono juhudi za Rais Samia kwenye Sekta ya michezo Nchini 

Mtumishi wa Mungu Baba Askofu Kutta anatekeleza kuwa pamoja na kuunga mkono Ilani ya Uchaguzi ya CCM kupitia imani ya kiroho.

"Sisi kama Kanisa la Anglikan Episcopal church Jimbo la Tanzania tutajikita zaidi katika kusaidia jamii husasani zilizopo pembezoni kwa kutumia kanisa tutawekeza katika huduma za kijamii kama Afya, Elimu na Maji kwa lengo la kuwaletea maendeleo waumini katika eneo husika pamoja na jamii yote kwa ujumla". Alisema Askofu KUTTA. 

No comments