Breaking News

KANISA JIPYA LA ANGLIKANA LA "EPISCOPAL ANGLICAN PROVINCE TANZANIA" (EAPT) KUZINDULIWA SEPTEMBA 15 JIJINI DODOMA

Kanisa jipya la Anglikana litakalojulikana kama Episcopal Anglican Province Tanzania (EAPT) linatarajiwa kuzinduliwa rasmi Septemba 15, 2024 Kongwa jijini Dodoma.

Akizungumza jijini Dar es salaam Askofu wa kanisa hilo, Elibariki Kutta amesema kuanzishwa kwa kanisa hilo jipya hakumaaanishi kuwa kanisa la Anglikana limemeguka, bali linatanua wigo kwa waumini kutawapa chaguo waumini wote wa Anglikana kuamua waabudu kuamua wasimame na imani ipi kati ya kanisa hili jipya na lililopo nchini

"Kanisa hili linakuja kurejesha na kusimamia misingi ya Kanisa la Anglikana kama ilivyokuwa miaka 60 kwani Anglikana haijameguka. Ni moja, ila uhuru wa wewe unataka kuwa na mtazamo gani au njia ipi katika maono yako,". Alisema Askofu Kutta.

Alisema lengo la ujio wa kanisa hili jipya ni kutaka kushikilia misingi, na kutunza imani iliyo safi ya kanisa la Anglikana na si mpya ni ileile iliyopanda uanglikana tangu kabla ya uhuru hadi mwaka 1965 na si kweli kuwa tunapinga imani iliyopo, bali tunakuza imani hii.

Askofu Kutta aliongeza kuwa ujio wa kanisa hilo utasaidia Serikali katika kuboresha utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii kupitia sadaka za waumini wanazotoa waumini katika maeneo wanayoabudu.

Amesema kupitia sadaka hizo waumini watakuwa na uwezo wa kuamua nini wafanye na kipi kiwe kipaumbele chao hususani katika uboreshaji huduma katika maeneo yao, ikiwemo kuanzisha vituo vya afya.

"Kupitia sadaka zao waumini watakuwa na uwezo wa kuamua nini wafanye kwa ajili ya kuboresha huduma katika maeneo yao, ikiwemo kuanzisha vituo vya afya, Maji, Elimu pamoja na shughuli mbalimbali za kiuchumi". Alisema Askofu Kutta.

Alisema Miradi hiyo itamilikiwa na waumini wa eneo hilo na kila sehemu ambayo kutakuwa na kanisa letu tutahakikisha jamii inafaidika kupitia huduma mbalimbali za kijamii zitakazoanzishwa waumini na wananchi wa eneo hilo ndio watakuwa wasimamizi wakuu.

No comments