JKT HAKUNA VITENDO VYA UONEVU - KANALI KOLOMBO
Kanali Kolombo akiwa na mmoja ya mhitimu wa mafunzo ya mujibu wa sheria Oparesheni miaka 60 iliyofanyika Kikosi 830 KJ Kibiti Wilayani Rufiji Mkoani Pwani.
Na Mwandishi Wetu Kibiti
NAWAOMBA wazazi ambao mmefika hapa leo kuwaona watoto wenu wakihitimu mafunzo ya kwamujibu wa sheria Oparesheni miaka 60 ya Muungano muende mkawe mabalozi wetu kwa wazazi wengine wawaruhusu watoto wao kujiunga namafunzo haya .
Ifahamike kwamba kijana anapojiunga na mafunzo ya kwa mujibu wa sheria ni kwamba huku hakuna uonevu wa aina yeyote mtawashuhudia vijana wenu pindi mtakapokuwa nao majumbani mwenu wakirudi kwani wamebadilika tabia na mienendo mbalimbali waliyokuja nayo, hapa wamefundishwa kuwa watii, wavumilivu katika changamoto mbalimbali watakazokutana , ujasiriamali na ubunifu.
" Kuna habari za hivyo zinaendele huko mitandaoni kwamba vijana wakijiunga JKT kuna maovu yanatendeka siyo kweli huu ni uvumi ambao unasambazwa na watu wachache ambao hawana uzalendo na nchi yetu" amesema Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Kolombo 06.Septemba, 2024 katika sherehe ya kufunga mafunzo kambi ya 830KJ Kibiti Wilayani Rufiji Mkoani Pwani.
DC Kanali Kolombo amewaasa wahitimu hao wa mafunzo ya kwa mujibu wa sheria oparesheni miaka 60 ya Muungano ya kikosi 830 KJ Kibiti kuzingatia kiapo walichoapa kuwa watakuwa watiifu, shupavu pamoja na kuyafanyia kazi mambo yote waliyofundishwa wakati wa mafunzo yao ya miezi mitatu.
"Pamoja na kwamba leo mmehitimu mafunzo yenu ya miezi mitatu kwa mujibu wa sheria mnapaswa muende mkatii kiapo chenu kwani mnavyoondoka hapa tambueni kwamba tayari mko katika mfumo wa orodha ya vijana waliopita JKT maana yake ninyi ni wazalendo hivyo kila mmoja aondoke hapa huku akikumbuka alivyo apa leo" amesema Mhe. DC Kanali Kalombo.
Kanali Kolombo ameroa shukran za dhati kwa Mkuu wa Kikosi cha 830 KJ Kanali Mohammed Bashiri Karuma amesema ameshuhudia namna vijana walivyo onesha kuiva kimafunzo hata wale ambao wamejaribu kutoroka nao pia wameiva.
Wakati huohuo ametoa shukrani zake za dhati kwa Mkuu wa Majeshi CDF Jacob John Mkunda kwa kutoa maelekezo ya kuboresha mafunzo hayo ambayo yametekelezeka.
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Brigedia Jenerali Solitina Bernad Mshushi amewapongeza vijana wote kwa kukubali kuja kujifunza mafunzo haya ya kwa mujibu wa sheria kwa sababu kwa kufanya hivyo wamejitende haki wenye na katika jamii waliyotoka na taifa kwa ujumla.
Mwakilishi wa Mkuu wa JKT Kanali George Barongo Kazahura amewasisitiza wahitimu hao kuzingatia kuzitunza afya zao ikiwa ni pamoja na kujiepusha na makundi yasiyo faa kwa sababu JKT haitafurahishwa kusikia kijana aliyepata mafunzo yake kwa mujibu wa sheria akikutwa kwenye vilabu vya gongo kujiunga na makundi yasiyofaa na yanayofanya vitendo vya utovu wa nidhamu.
No comments