Breaking News

FIGO MARATHON MSIMU WA TATU KUFANYIKA SEPTEMBA 22 DAR

Mkurugenzi wa huduma za Tiba Wizara ya Afya Dkt. Hamad Nyembea leo Septemba 5, 2024 amekutana na Taasisi ya The Healthier Kidney Foundation ambao ni waandaaji wa Figo Marathon.

Katika mazungumzo yao Dkt. Nyembea ameipongeza Taasisi ya The Healthier Kidney Foundation kwa kuhamasisha jamii kufanya mazoezi ili kujenga taifa lenye afya imara na kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza hususani Figo.

"Wizara inaendelea kushirikiana na wadau  ili kubadili mitindo ya maisha ambayo ni hatarishi  na kuwa na jamii yenye ustawi bora wa afya kwa kufanya mazoezi.

Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Jenipher Mambo pamoja  na Mkurugenzi wa Programu wa Taasisi hiyo Maulid Juma wamefanikiwa  kuzindua sare rasmi za Figo Marathon kwa Msimu wa tatu zitakazofanyika Septemba 22, 2024 Jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.

Taasisi ya The Healthier kidney Foundation Kupitia Mbio za Figo Marathon 2024 imeazimia, kupeleka sehemu ya Mapato hayo kuboresha huduma za Afya nchini na  kusaidia matibabu ya watoto wapatao 50 wenye changamoto za magonjwa ya Figo .

No comments